ninapoitazama hiyo picha, naona utajiri wa mali, utamaduni na tabia.
Angalia afya ya watoto pichani; ni njema tu, wamekula na kushiba
Angalia nyuso zao za furaha na confidence ya kaka yao
Angalia utajiri kwa kigezo cha kununua misumari iliyogongelewa kwenye hiyo chanja waliokalia, palipo na uwezo wa kununua misumari, hapakosi wa kununua nguo na sabuni
Angalia nguo, hazijachakaa
Angalia utamaduni wa kujipamba, hizo shanga shingoni, thamani yake ni kubwa mno, kama ni suala la nyumba, huo ndio utamaduni wa watu hao. Kama ni watoto kukaa uchi, well inawezekana ni kutokana na utoto wao na michezo walokuwa wakicheza kabla ya kupigwa picha hiyo, tena michezo yenyewe ndo imewafanya wajae mavumbi. Kimsingi sio wachafu, ndo maana wamenyolewa nywele vizuri sana.
Angalia heshima aliyopewa/alojipa mtoto wa kike; kujisetiri. Hii ni kinyume na tamaduni za magharibi ambapo anayejisetiri ni mwanaume, wanawake uchi uchi (kumradhi)
Kwa ufupi, kama mpiga picha alitaka kuzungumzia umaskini, mwambie sio hivi. Data hazijatosha arudi field.