Yanaweza kuwepo japo si lazima. Mwanamke wa namna hii huwa anajiandaa kuishi peke yake hata wakati yupo na wewe. Si ajabu akawa anafanya maamuzi mwenyewe bila kukushirikisha au kukutaarifu kwa kuwa hajazoea kuona mama yake akiitafuta ridhaa ya mwanaume kabla ya kufanya jambo.
Ni masuala tu ya kisaikolojia ambayo hata mwanaume aliyelelewa na baba mkorofi mwenye kumpiga mama, hubeba mentality ya kuwa ili uwe mwanaume lzm wanawake waliopo around you wawe taabuni wakati wote.
Ila kwa namna nyingine yaweza ikawa nzuri kwako pia. Mwanamke aliyekosa upendo wa baba, anaweza akawa safi zaidi kwako if you are caring person. Ni dhahiri atahitaji kufidia aliyoyakosa kwa baba toka kwako, kwa hiyo akawa msikivu na mwambata kwa kila hali.