kuna chama kinaitwa Chakuhawata na kingine Chakamwata.
Ila mwalimu inabidi uwe smart, usijiunge na chama kwa sababu kina ada ndogo halafu hakina uwezo wa kukuhudumia. Tumia akili zako vizuri.
Mwalimu gani huyo anakuwa mvivu wa kufuatilia mambo kwa undani na kuyaelewq.
Walimu hata huku Katavi wengi haturidhishwi na utendaji wa cwt hivyo may 2025 tulijaza form kujitoa cwt na kujiunga na chakamwata. Danadana katika ofisi za utumishi zinakera. Mara mtandao hakuna, mara hatuna password mara subirini kdg mara subirini mwezi ujao. Kimsingi hata mtoto huwezi ukamdanganya hivyo.
Matokeo yake tunaendelea kukatwa cwt huku nao cwt wakisema hatuwatambui kwa kuwa mlijaza form nyingine lakini makato wanachukua. Mwaka na mwezi umeosha. Inakera na kukatisha tamaa ya kazi