Mecco Sports Club

Mecco Sports Club

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
1665502692644.png

Kikosi kilikuwa na;

George Mangula

Rashidi Mandanje

Gabliel Mwintika

Mbaga Mwantiku

Charles Makwaza

Dannifon Ngesi

Abeid Kasabalala

John Moses Kanyiki

Betwely Africa

Efeam Kayeta

Nassibu Abbasim

Wachezaji wengi Juma Ahmad, Nurdin Kasabalala, nk

Mnyama alikula 3 mtungi Mbeya na Yanga kala 1 bila Mbeya. Walivyokuja Dsm Simba yanga wote walidroo.
 
Tulioanza kusikiliza mpira kipindi cha Ahmed Jongo hatuna namna
Huyu mwamba anakutangazia mpira utadhani unaona vile na kuwafahamu wachezaji kwa kuwaona kumbe unasikia.

Kule kanda ya ziwa alikuwepo Dominic Chilambo, huyu jamaa aliipamba Pamba na nahisi ushawishi wake uliifaanya Pamba iwe tisho ligi kuu.

Wana TP Lindanda Kawe Kamo😍
 
Ahmed Jongo ndani ya Lusaka, anatangaza ile mechi dhidi ya Kk ,hatutakuja kupata Taifa stars kama ile...ndani ya Lagos kwa wapopo, President kaunda (rip)hakuamini kilichotokea mbele yake,Peter Tino anapiga mpira wa kichwa na kujaa wavuni, eti leo mchezaji wangu wa timu ya taifa yupo kiselule kisa chips mayai zimezidi!
 
Hiki kikosi si ndiyo kiliikimbia yanga kipindi Cha pili!
Sidhani, ilikuwa 1991 au 1992 nahisi. Maana Simba walikuwa Tabora. Mpaka saa 6 au 7 mchana siku ya mechi walikuwa Tabora Hotel maana mimi pia nilikiwepo hapo Jirani. Tulijua hawaendi kucheza maana nao pia walikuwa wanalalamika tu kama Yanga ya sasa kila kitu kulalamikia TFF. Sasa saa 10 tukasikia wametia timu uwanjani, mara kipindi cha pili hawakurudi uwanjani
 
Huyu mwamba anakutangazia mpira utadhani unaona vile na kuwafahamu wachezaji kwa kuwaona kumbe unasikia.

Kule kanda ya ziwa alikuwepo Dominic Chilambo, huyu jamaa aliipamba Pamba na nahisi ushawishi wake uliifaanya Pamba iwe tisho ligi kuu.

Wana TP Lindanda Kawe Kamo😍
Tupweisa Lindanda
 
Si ndiyo 92 Simba walikimbia,propaganda wakadai refa aliwaambia sharti wale za kutosha
 
Ahmed Jongo ndani ya Lusaka, anatangaza ile mechi dhidi ya Kk ,hatutakuja kupata Taifa stars kama ile...ndani ya Lagos kwa wapopo, President kaunda (rip)hakuamini kilichotokea mbele yake,Peter Tino anapiga mpira wa kichwa na kujaa wavuni, eti leo mchezaji wangu wa timu ya taifa yupo kiselule kisa chips mayai zimezidi!
Kweli Kiswahili kigumu aisee
 
Huyu mwamba anakutangazia mpira utadhani unaona vile na kuwafahamu wachezaji kwa kuwaona kumbe unasikia.

Kule kanda ya ziwa alikuwepo Dominic Chilambo, huyu jamaa aliipamba Pamba na nahisi ushawishi wake uliifaanya Pamba iwe tisho ligi kuu.

Wana TP Lindanda Kawe Kamo😍
Sidhani kama alipata mrithi sahihi. Nkamia alijitahidi kidogo
 
Ahmed Jongo ndani ya Lusaka, anatangaza ile mechi dhidi ya Kk ,hatutakuja kupata Taifa stars kama ile...ndani ya Lagos kwa wapopo, President kaunda (rip)hakuamini kilichotokea mbele yake,Peter Tino anapiga mpira wa kichwa na kujaa wavuni, eti leo mchezaji wangu wa timu ya taifa yupo kiselule kisa chips mayai zimezidi!

Peter Tino: Shujaa wa Stars aliyeyumba kiuchumi-1​

tino.jpg

Summary​

Katika toleo hili tunakuletea makala ya mwanasoka mwingine nyota wa zamani, Agustino Peter aliyezoeleka mbele ya mashabiki kwa jina la Peter Tino ambaye alitamba miaka ya 1980 na 1990 mwanzoni.
KATIKA moja ya matoleo yetu ya mwezi uliopita, tulikuletea makala ya mwanasoka wa zamani, Jellah Mtagwa aliyekuwa nahodha na beki wa timu ya Taifa na klabu ya Pan Africa ya Dar es Salaam.

Makala ile ilikuwa sababu ya kuibua mjadala bungeni baada ya Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan kuhoji iwapo serikali ina utaratibu wowote wa kuwasaidia wanamichezo wa zamani.
Hata hivyo, Serikali kupitia Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala ilitoa ufafanuzi kuwa hakuna fungu kwa ajili ya wanamichezo hao walioiletea nchi sifa.
Katika toleo hili tunakuletea makala ya mwanasoka mwingine nyota wa zamani, Agustino Peter aliyezoeleka mbele ya mashabiki kwa jina la Peter Tino ambaye alitamba miaka ya 1980 na 1990 mwanzoni.
Soka Mei 07, 2013
Tino katika maisha yake ya soka la ushindani alikuwa mshambuliaji tegemeo wa timu za Taifa (Taifa Stars) na klabu za Pan Africa, Yanga na Majimaji ya Songea.
Hadi anaamua kutundika daruga, Tino alijijengea heshima katika medani ya soka kutokana na umahiri wake wa kuzifumania nyavu lakini kwa wakati huu hali yake ya kiuchumi iko hovyo.
Kielelezo cha hali ngumu ya kiuchumi kinajidhihirisha katika harakati za kukutana na Tino baada ya kuambiwa kwamba wakati mwingine hana hata simu ya mkononi.
Mtu wa kwanza kumuomba msaada wa kukutana na Tino ni mdogo wake, Gebo Peter, huyu naye enzi zake alitamba na timu za Sigara na Simba akiwa mshambuliaji kabla ya kutundika daruga.
Baada ya kumueleza Gebo nia yangu na kumuomba namba ya simu ya Tino, alinijibu: “Sina uhakika kama simu niliyomuona nayo siku kadhaa zilizopita bado anayo, lakini nikifika nyumbani nitakuchukulia namba yake kisha nipigie nitakupa kama atakuwa bado yupo hewani.”
Majibu ya Gebo yananifanya nitumie mbinu nyingine, naamua kwenda anapoishi Tino maeneo ya Vingunguti jijini Dar es Salaam.

Kwa msaada wa shabiki mmoja wa soka nafika eneo la Vingunguti hiyo ni baada ya madereva kadhaa wa pikipiki wa eneo hilo kuonyesha kushangaa maana jina hilo ni geni kwao.
Hata hivyo kijana mmoja wa makamu ananifahamisha kwamba huwa anamuona lakini hana uhakika anakaa wapi na baada ya kuhangaika hatimaye nafanikiwa kufika nyumbani kwa Tino.
Nakaribishwa na mwanaye lakini ananiambia baba yake hayupo na zaidi ya hilo akakataa kunipa namba ya simu jambo ambalo linaongeza ugumu wa kumpata Tino.
Kwa bahati anatokea mtu ninayemfahamu nikiwa maeneo hayo hayo na baada ya kumueleza shida yangu akanipa namba ya Tino ndipo nilipompigia naye akapokea na kujibu: “Njoo nyumbani nipo.
Ninapofika tu Tino naye anakuja akitokea ndani ya nyumba ambayo pia anaishi ndugu yake Gebo. Naikumbuka sura ile ile ya mwanasoka wa zamani ingawa anaonekana katika hali ya utu uzima.
Pamoja na mafanikio ya kujivunia katika soka, mambo ya Tino kiuchumi hayajakaa sawa, lakini nje ya hilo, wino ulioandika historia ya mafanikio ya Tino ni kama umefutika.
Tino alitamba enzi za wakali wengine waliosifika duniani kina Diego Maradona wa Argentina, Karl-Heinz Rummenigge wa Ujerumani na wengine ambao majina yao yameandikwa kwa wino usiofutika katika klabu na timu zao za Taifa na wameendelea kuwa gumzo hadi hii leo.
Kwa Tino hali ni tofauti, jina lake limeandikwa kwa wino ambao umefutika si katika timu ya Taifa hata klabu alizochezea wako mashabiki na hata viongozi ambao hawajui Tino ni nani achilia mbali mahali aliko na anachokifanya.

Katika mazungumzo yetu, Tino anakiri mwenyewe kwamba hali yake ya kiuchumi si nzuri lakini anaeleza zaidi sababu ya hali hiyo.
“Ukweli ni kwamba soka la wakati wetu lilikuwa hiyari ya moyo, wachezaji walicheza kwa mapenzi yao na kutafuta utukufu na heshima na wala si kipato kama ilivyo sasa,’’ anasema Tino.
Tino aliyeiwezesha Tanzania kwa mara ya kwanza kucheza fainali za Mataifa ya Afrika nchini Nigeria mwaka 1980 anakiri kwamba yupo kama hayupo ingawa ana malengo ya kuwekeza kwa kile anachokijua kuhusu soka la Tanzania.
“Natafuta timu ya watoto ili niwafundishe soka, hilo ndilo ninalotaka kufanya,’’ anasema katika hali ya kujiamini.
“Nimelitumikia soka la Bongo kwa moyo mmoja lakini sina cha kujivunia zaidi ya heshima na bahati ya baadhi ya watu kunikumbuka na wakati mwingine TFF kunialika katika hafla tofauti.
“Kuna wakati niliitwa kuzungumza na timu ya vijana ya U-17 na hata Stars, hiyo inanipa faraja lakini siwezi kusema nina kitu kinachoonekana ambacho naweza kujivunia kuwa hiki kimetokana na utumishi wangu wa zaidi ya miaka 15 katika soka,” anasema.
Alipotokea
Mchezaji huyo mkongwe alizaliwa mwaka 1956, jijini Dar es Salaam, akiwa mtoto wa tano katika familia ya watoto tisa ya Mzee Peter Agustino.
Alianza kucheza soka mwaka 1967 akiwa na timu za mtaani, Bonde FC na baadaye Young Kinya za Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Anasema kuwa baada ya kuchezea timu hizo na nyingine za mitaani mwaka 1974 alisajiliwa na klabu ya soka ya Kiwanda cha Nguo cha Urafiki ambayo ilikuwa inashiriki Ligi Daraja la Tatu.

Akiwa katika timu hiyo alikutana na wakali wengine wa soka kama Awadhi Gesani ambaye baadaye alienda Sunderland (Simba) na Gibson Sembuli.
Wengine anawataja kuwa ni Abdulrahman Juma, Adam Juma na wengineo ambao anasema walikuwa wakubwa kwake kiumri ambao anasema walimtia moyo na kumfanya ajifunze mengi kutoka kwao.
Hakudumu katika timu hiyo ambayo pia ilikuwa imempa ajira katika Kiwanda cha Urafiki.
Baadaye alijunga na timu ya Kiwanda cha Nguo cha Mwatex, Mwanza ambayo anasema ni kama alipita kwani aliitumikia kwa muda mfupi kabla ya kutua Kurugenzi ya Arusha na baadaye African Sports ya Tanga.
Akiwa na timu hiyo alikutana na wachezaji kadhaa waliokuwa wanang’ara katika klabu hiyo na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’.
“African Sports naweza kusema ndiko nilikocheza mpira na kuonekana, watu kama Kassim Mwabuda, Omary Bawaziri, Mhando Mdeve na wengineo walinipa changamoto iliyonifanya nijitambue na kujua wajibu wangu uwanjani.
Akiwa African Sports mwaka 1977 ndipo alipoitwa kuunda timu ya Taifa na kudumu nayo hadi mwaka 1985 huku akishiriki mashindano mbalimbali na hata Pan Africa walipomhitaji alikuwa tayari ana namba Taifa Stars .
“Nilijiunga Pan African mwaka 1980 na niliichezea misimu minne kabla ya kuhamia Majimaji ya Songea na baadaye Yanga hadi nilipostaafu soka mwaka 1991 baada ya kuona siwezi tena kumudu mikikimikiki ya uwanjani.

Unazi na tuhuma za kupanga matokeo
Tino anasema tofauti na wakati huu kipindi hicho kuna wachezaji ambao walikuwa wanadaiwa kuzichezea timu nyingine wakati mapenzi yao yakiwa ama Yanga au Simba na hali hiyo anasema wakati fulani ilimgharimu kwani kutokana na mapenzi yake Yanga alikuwa anapata tabu kidogo kuifunga.

“Nilikuwa naweza kuwamaliza mabeki wote na nikabaki na kipa lakini sijui inakuwaje najikuta nashindwa kuifunga Yanga,” anasema na kuongeza kuwa hilo hata baadhi ya viongozi wa klabu alizokuwa anachezea walilijua na wakati mwingine alinyimwa namba katika mechi dhidi ya Yanga.
Makocha walikuwa wanamuweka benchi hali ambayo hakuwa anajali ingawa ilikuwa inamuumiza bado hakutaka kupingana na mawazo ya wengi.
“Hata nikikosa bao kwa bahati mbaya naambiwa aaaaaaaah yule hawezi kuifunga Yanga,” anasema Tino na kuongeza kuwa zama hizi hakuna unazi kama zamani isipokuwa kuna biashara kwa maana kuwa kipindi hicho watu walikuwa wanafanya unazi kwa mapenzi yao ya moyoni kwa klabu lakini zama hizi mechi zinauzwa.
Anafafanua kwamba kwa zama hizi unajua kabisa matokeo kabla ya mechi hali ambayo anasema inachangiwa na wachezaji kutokuwa na ajira nyingine na waamuzi kugeuza filimbi ndio mtaji wao.
Tino anatoa mfano wa matokeo ya mechi ya karibuni iliyochezwa Tanga bila ya kutaja jina la timu ambayo anasema matokeo yake yalivuja kabla mechi haijachezwa.
Tino anasema kwa zama hizi klabu zinapanga matokeo na waamuzi ambao wamepoteza dira kwa kuchukulia uamuzi ndio ajira na wanataka kuishi kwa kutumia filimbi na hivyo kupindisha maamuzi kumridhisha aliyemhonga.
“Refa anaamua kufumba macho na kutoa kadi nyekundu zisizo na mashiko au hata kutoa bao na penalti wakati mwingine ili kuhalalisha bahasha aliyopewa,” anasema.
Tino anasisitiza kuwa kwa soka la namna hiyo nchi haiwezi kufika popote licha ya jitihada zinazofanywa na baadhi ya wadau.

“Kuna ukweli kuwa waamuzi wengi hawana ajira na mbaya zaidi wapo katika ratiba za mechi, wanajua mechi zao mapema hali inayotoa mwanya wa rushwa na upangaji wa matokeo,’’ anasema.
Anaongeza kuwa wakati wao miaka ya 1980 mwamuzi wa mchezo alikuwa anajulikana siku ya mkutano wa kabla ya mechi (Pre- match meeting), unaofanyika siku hiyo ya mchezo tofauti na wakati huu ambao mwamuzi anajua mechi yake wakati mwingine wiki mbili kabla.
“Mwamuzi akishajijua ndiye anayesimama katika mechi fulani kubwa kitu anachofanya ni kujipitisha kwa matajiri wa klabu na kuwakumbusha kuwa yeye ndiye atakayesimama kati hivyo wafanye maarifa vinginevyo wasije wakamlaumu,” anasema.
 
Back
Top Bottom