Mechi gani ya Simba na Yanga, Yanga walimpiga Refa

Rambo man

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2022
Posts
243
Reaction score
364
Kuna mechi ya simba na yanga nakumbuka wachezaji wa Yanga walimpiga refa, naomba nikumbushwe refa aliyepigwa na wachezaji walipiga na kwa sababu gani
 
Ni Israel Nkongo Mujuni na hii ni baada ya Uto kukandwa vilivyo goli 3-1 na Azam FC katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

RAI YANGU KWA TFF: Hawa Uto ukiwakanda goli nyingi huwa wanageuka mabondia. Chonde chonde muongezeeni ulinzi Refa wa mechi ya 23/10, Ndg. Ramadhani Kayoko kwani anafamilia na inamtegemea.
 
kuna mechi ya simba na yanga Nakumbuka wachezaji wa Yanga walimpiga refa, naomba nikumbushwe refa aliyepigwa na wachezaji walipiga na kwa sababu gani
"Tefa" ni nini? Simba mna ujinga usiomithilika.
 
Kuna mechi ya simba na yanga nakumbuka wachezaji wa Yanga walimpiga refa, naomba nikumbushwe refa aliyepigwa na wachezaji walipiga na kwa sababu gani
Una umri gani wewe kwa sasa mpaka kutaka kukumbushwa mechi iliyochezwa miaka michache tu iliyopita?
 
Kwani We Unafikiri Yule Bondia Kwenye Nembo Ya Yanga anamaanisha Nini..?
Utopolo Wagomvi haoo..!

Ndani ya Uwanja wanae muanzisha Ugomvi Morisoni.
 
Kwa sisi Yanga ngumi zipo.
Mandonga [emoji116]huyu hapa.
 
Kuna beki wa yanga anaitwa mwansika nduye alimpiga mwamuzi,alilaaniwa akapotea mazima kwenye soka
 
Hahahah kitu ipo kwenye chata hapo. Jasiri haachi asili
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] nimecheka sana. Ila hawa waamuzi wetu Kuna wakati kipigo ndio inafaa kuwa adhabu yao maana Kwa madudu wanayoyafanya uwanjani na TFF wanaishia kuwafungia mechi tatu.. Huku timu imepoteza point 3 kwa upumbavu wao
 
Kwani We Unafikiri Yule Bondia Kwenye Nembo Ya Yanga anamaanisha Nini..?
Utopolo Wagomvi haoo..!

Ndani ya Uwanja wanae muanzisha Ugomvi Morisoni.
juzi tu naskia walimpiga shabiki wa simba
 
hapa yanga walikuwa hawana hela ya kuwaonga marefa ndio maana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…