La Quica
JF-Expert Member
- Dec 19, 2017
- 1,009
- 2,315
Hakuna mechi ya mpira iliyochezwa kwa mda mrefu kuliko ile ya Marekani na Argentina mwaka wa 1941 na ilikuwa fainali,wanaume walipiga dakika 90 ikawa ni sare 2-2 refa Tom Foll akaongeza zingine 30 bado ikawa vilevile,wakaenda kwenye matuta za kwanza 5 wakatoka 4-4 refa akaongeza zingine hadi 150 bado ikawa sare wachezaji wakawa wamechoka wakaambiwa waende wapumzike,baada ya mda wakarudi na kuendelea na penalti hadi zikafika 800 bada wakawa wako sare kumbuka hii ni fainali mshindi lazima, kuendelea usiku ukaingia ikabidi mashabiki na wachezaji walale uwanjani hadi asubuhi,kesho yake penalti zikaendelea lakini wapi,wakaamua walete shilingi warushe juu iamue mshindi maajabu shilingi kurushwa juu kuanguka chini ikasimama wakafanya hivo mara tano bado ilikuwa inasimama tu hadi wakaamua wakate kombe katikati wagawane nusu nusu
Sijawahi wadanganya ndo mara yangu ya kwanza kufanya hivo sitarudia.
Haiwezekani nidanganywe peke yangu..Niwatakie Jumanne njema
Sijawahi wadanganya ndo mara yangu ya kwanza kufanya hivo sitarudia.
Haiwezekani nidanganywe peke yangu..Niwatakie Jumanne njema