Mechi kati ya Namungo na Mbeya Kwanza yaahirishwa baada ya ambulance kuchelewa uwanjani

Mechi kati ya Namungo na Mbeya Kwanza yaahirishwa baada ya ambulance kuchelewa uwanjani

denooJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
18,509
Reaction score
68,228
Yale maajabu ya mpira wetu wa bongo yameendelea baada ya mechi ya NBC Premier League, kati ya Namungo na Mbeya Kwanza, kuahirishwa sababu ikiwa ni ambulance kuchelewa kurudi uwanjani.

Uongozi wa Namungo umejitetea kwa kusema halmashauri ina ambulance moja, hivyo kutokana na gari hilo la kubebea wagonjwa kumpeleka mgonjwa hospitali, lilichelewa kurudi ili kuuwahi mchezo huo uliokuwa upigwe jana.

Kwa sasa inasubiriwa taarifa kutoka TFF ili kuona kama mchezo huo utapangiwa tarehe nyingine, au kama patakuwa na maamuzi yoyote mengine tofauti.
 
Hakuna kupangwa tarehe nyingine, Mbeya kwanza wapewe point zao 3 na magoli 3
 
Hakuna kupangwa tarehe nyingine, Mbeya kwanza wapewe point zao 3 na magoli 3
Kikanuni Mbeya Kwanza watapoteza points kwasababu Ambulance iliingia uwanjani saa 16:24 muda ambao kikanuni mchezo ungetakiwa kuendelea lkn bado wakagoma kuendelea na mchezo.
 
Kikanuni Mbeya Kwanza watapoteza points kwasababu Ambulance iliingia uwanjani saa 16:24 muda ambao kikanuni mchezo ungetakiwa kuendelea lkn bado wakagoma kuendelea na mchezo.
Ebu weka hiyo kanuni inavyosema mkuu
 
Hakuna kupangwa tarehe nyingine, Mbeya kwanza wapewe point zao 3 na magoli 3
Kwa akili ya kawaida hii ndio solution, ila ngoja tusubiri tuone labda kuna wazo tofauti..
 
Kikanuni Mbeya Kwanza watapoteza points kwasababu Ambulance iliingia uwanjani saa 16:24 muda ambao kikanuni mchezo ungetakiwa kuendelea lkn bado wakagoma kuendelea na mchezo.
Wazo la tofauti ndio kama hili, kama ikithibitika hao jamaa walipeleka ambulance saa 16:24 jioni kabla ya muda wa kugoma kisheria kufika, basi Mbeya Kwanza inaweza kuwa cost kwa kugoma kwao.
 
[emoji849][emoji849][emoji849]
Screenshot_20220517-162304_Instagram.jpg
 
Nimeridhishwa na hukumu Ila sijafurahishwa na adhabu ni kubwa mno. Mbeya Kwanza walisitahili kuadhibiwa Kwa utoto waliooneshwa maana Kwa vyovyote kosa la kutokuwepo Ambulance si la Namungo kama timu Bali la management ya soka maana Ambulance siyo ya Timu ni ya serikali.

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom