Mechi ligi Kuu Bara: Mbao FC na Simba SC zatoshana nguvu, Kirumba

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971


Mashabiki wa soka jijini Mwanza wamefurika kupanga foleni kwa jili ya kuingia uwanjani ili kuishuhudia mechi ya Simba na Mbao FC inayotarajiwa kupigwa leo kwenye dimba la CCM Kirumba jijini hapa.

Mechi hiyo yenye ushindano inatarajiwa kuchezwa leo Alhamisi saa 10 jioni, huku mashabiki wakiwa nje ya uwanja kabla ya mageti kufunguliwa.

Je, Simba ataweza kuiangamiza Mbao leo?

Tuungane kwa Live Updates
===============================================
Mbao FC
(Kiyombo 46', Maganga 81') 2 - 2 (Kichuya 16', Kotei 49') Simba SC

Kikosi cha Simba SC

Manula, Nyoni, Tshabalala, Juuko Mwanjale, Kotei, Mzamiru, Gyan, Bocco, Okwi, Kichuya

Sub za Simba SC
Emanuel Mseja, Ally shomary, Salim Mbonde, Mkude, Ndemla, Niyonzima, Juma Luizio.

Kikosi cha Mbao FC
Kelvin Igendelezi, Boniphace Maganga, Abubakar Ngalema, Yusuf Mgeta, Yusuph Ndikumana, Sadala Lipangile, Ibrahim Njohole, Hussen Kassanga, Moses Shabani, Said Seid, Habibu Kiyombo

Kikosi cha Akiba cha Mbao Fc
Kabally Swaleh, James Msuva, Herbet Lukindo, Daud Mwasa, Amos Charles, Ndaki Kisambare, Emmanuel Muvyekore

Mechi Imeanza sasa
01' Simba ndio wanaanza mpira, Okwi na Bocco wakianza katikati pale
02' Mpira bado umetulia kila mtu akionekana kumsoma mwenzake
04' Hussen Kassanga anajaribu kutoka mbali lakini inakuwa ni goli kick kwa upandea wa Simba
08' Bado mpira unachezwa zaidi eneo la katikati kila timu inajaribu kucheza kwa tahadhari ikijaribu kumsoma mwenzake
09' Emmanuel Okwi alijaribu kupita kutokea pembeni hapa lakini akamchezea faulo beki wa Mbao nje kidogo ya box la Mbao

11' Ilikuwa hatari eneo la golini kwa Simba. Mbao wamepoteza nafasi hapa, wamegonga mwamba kwenye goli la Simba
15' Ibrahim Njohole anamkata na kumueka chinin mzima mzima Kotei.

16' Goooooooooooooal Simba wapata Goal. Kichuya
Erasto Nyoni alimimina krosi nzuri iliyomkuta Kichuya, ambaye amejinyanyua na kupiga kichwa kizuri kilichomshinda mlinda mlango wa Mbao, Kelvin

17' Kumekucha sasa CCM Kirumba, Mashabiki wa Simba wamenyanyuka wanashangilia na kuimba kwa shangwe nyingi.
21' Mbao wanakosa umakini sasa, baada ya kufungwa wanaonyesha kutokulia na mpira kabisa
25' Mbao wanakaa nyuma sasa na kujaribu kuchambulia kwa kutumia mipira mirefu,
29' Mpira umesimama; James Kotei anasililizia maumivu chini hapa, madaktari wanaingia uwanjani na umpa huduma. wakati huo huo makocha wa timu wanatumia nafasi hiyo kutoa maelekezo wa timu
30' Mpira unaendelea sasa

34' John Bocco anachezewa faulo pembeni kabisa mwa uwanja
Simba wanapiga faulo hiyo, lakini Muzamiru anaachia shuti kali kabisa hapa na kuwa ni goal kick

37' Mabadiliko kwa upande wa Mbao FC
Said Seid anatoka na Herbet Lukindo anaingia

39' Simba wanapata faulo, Kichuya anachezewa rafu
Okwi anapiga faulo hiyo lakini inakuwa ni goal kick

45' Dakika 4 zinaongezwa kabla ya kuenda mapumziko

45+3' Shiza Kichuya ameumia na kushindwa kuendelea na Mpira, anatolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Haruna Niyonzima

45' Kipindi cha pili mpira umeanza

46' Gooooooooooooooal Mbao wanasawazisha
Mbao FC wanasawazisha goal kupitia mkwaju mkali wa chini chini ulipigwa na Habibu Kiyombo na kumshinda gilikipa wa Mbao

49' Gooooooooooooooal Simba wanapata goal la pili
James Kotei anawapatia Simba goal la pili, aliugusa mpira akiwa ndani ya box ikiwa ni baada ya Nyoni kupiga mpira wa faulo, na kuipatia Simba goal la pili. Goal lake la kwanza kwenye historia ya timu ya Simba

58' Okwi anaachia mkwaju baada ya Simba kugongeana lakini hakulenga lango
59' Mbao FC wanafanya mabadiliko, wanamtoa Moses Shabani anatoka anaingia Ndani Kisambare

67' Mpira umetulia ukiwa simba nauchezea sana na kutaka kupanga mashambulizi mengine huku Mbao wakiwa wanacheza kwa kujihami kuzuia mipango

68' Simba wanapata faulo eneo zuri, sio mbali sana kutoka eneo la box la kumi na nane
69' Niyonzima anaachia mkwaju mkali kabisa nje ya 18, goal kick
74' Okwi anapitishiwa pasi nzuri kutoka nyuma lakini Mgeta anafanikiwa kuondoa mpira ule
75' Simba wanafanya mabadiliko; Juma Liuzio anaingia kuchukua nafasi ya Nicholas Gyan
77' Kumetokea vuta nikuvute kati ya Bocco na Ndikumana, Ndikumana nabaki chini akiwa anashika shika paji la uso akiashiria kuumizwa. Refa anasema Boco amecheza rafu
80' Mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja na Simba ndiyo wanaoumiliki zaidi na Mbao FC wakijaribu kufanya mashambulizi ya kushitukiza

81' Goooooooooooooooal Mbao wanapata bao la pili.
Boniphace Maganga awapatia Mbao FC goli la pili. Anapiga mpira mzuri wa juujuu kutoka nje ya box unamshinda Aishi Manula na kujaa kimiani

83' Simba wanafanya shambulizi kali kabisa lakini Mbao FC wanaonekana wako makini kabisa
86' Maganga tena anaachia mkwaju mkali sana hapa, Manula anadaka vizuri
88' Simba wanapata faulo nje ya D hapa, tuone itazaa nini faulo hii
89' Bocco anapiga faulo ile lakini kipa anasimama imara na kudaka vizuri mpira ule
90' Dakika 3 zinaongezwa hapa

90+3' Mpira umekwisha.
Simba SC na Mbao FC wanatoshana nguvu kwa kufungana magoli mawili kwa mawili
 
Huku Simba huku Barcelona

Raha saaaana japo Bongo Bahati Mbaya
 
mo ibrahim ata benchi hapangwi,duh inabidi tuwagawie mtani wetu wa jangwani awasaidie kwenye kiungo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…