Ukweli uko wazi Al Ahly ni Mlima mrefu sana kwa Simba ambayo ni underdog! Jana Al Ahly walifanya kama vile Chui akishamlegeza swala anaacha wanawe wacheze nae!! Swala akitaka kutoroka anamuwahi na kumtuliza Tena!!
Al Ahly walionesha wanauwezo wa kufunga goli muda wanaotaka na lengo lao Jana ilikuwa mechi iishe kwa suluhu tu wasiiaibishe Simba, Sasa Makolo walipokukuruka na kufunga goli jamaa wakaona hawa mbumbumbu watatuaibisha wakarudisha goli fasta na kuendelea na masihara Yao!!
Sote tulijua na tulishasema mechi za Simba super cup ni mbili tu ila Makolo walishupaza mishipa ya shingo!
Dume la Mamba halijawahi kusafiri peke yake, pembeni yake daima Huwa Kuna kenge wanamsindikiza huku wakimbebea mizigo yake!!
Huu ni muda Sasa tuhamie kuzungumzia Yanga tunacheza ijumaa na tawi letu la Singapore Big Stars ushindi ni kawaida tu!! Mambo ya Al Ahly yameisha kama tulivyotabiri, Makolokwinyo tupumzusheni na stori za kale za ligi ya wababe wa super cup!