Mechi ya Barcelona na Juventus leo Juni 5, 2015

Afadhali timu zote zilikuja kucheza mpira sio kama ile timu ya daraja la kigamboni inayokuja kuvizia-vizia kufunga goli afu wanaweka mpira kwapani
Ntuzu, Mentor
 
Hongera barca.. Timu bora kwangu ni juventus fc..

Wakati mwingine hata kama inakukera toa tu credit kwa anaejua. Kadri ilivyo level ya Barc ni kubwa kwa kila idara kwa Juve. Na kwa kutaka kusawazisha wakaacha goli lao na kujaa kwa adui. Sasa aina ya wachezaji wa Barc wako kamili kila idara kuanzia pasi hadi counter attack. Na angalia walivyo wajanja, ingekuwa team ya ovyo ingekuwa offside maana papara kidogo mmoja wa wachezaji angezidi bega ni offside, wakamtumia yule mchezaji mmoja wa Juve kwenye line moja na kupiga goli tarrtibuuuuuuu! Barca watamu hasa kwa mpira safi wenye pasi na faulu chache. Ukimkaba Messi atakufunga Suarez, ukimkaba Suatez atakufunga Neymar likewise Neymar ukimkaba ujue hata beki anakufunga. Kiufundi na kiumahiri Barcelona ni team bora duniani pamoja na Real Madrid!
 
Mbona mpira umeisha kienyeji?

Nilisema Mturuki kala chake mapema. Mpira umeisha kama vile mechi ya darasa la sita A na sita B kengele ya kurudi darasani inapopigwa.
 
Komredi hata kabla sijamaliza kuandika kuwa nataka Neymar atupie japo moja....kufumba na kufumbua naona nyavu ya Juve inacheza tena.

Comrade nitabirie siku ya kufa kwangu. Manake ulisema 3-1 na ikawa. We kijukuu cha mtume hakyamama...
 

uko sahihi mkuu
 
Fainali na utoaji wa zawadi bila ya uwepo wa Sepp Blatter!!
 
LOL Thomas Vermalean na yeye anadiriki kupokea medal....Nadhani jamaa hajacheza hata mechi moja tangu ahamie Barca
 
Hongera Barcelona,hope kila timu ilideserve kufika fainali na mshindi kapatikana,Barcelona
 
Ngoja tuone kama fundi Benitez atajibu mapigo mwakani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…