carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Mkutano wa wetu wa leo ni kuhusu mchezo wa hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC 15 de Agosto ambao utapigwa Oktoba 21, 2026 saa 9:00 alasiri katika Uwanja wa Uhuru. Mabadiliko ni kutoka kesho Jumanne kwenda Jumatano. Msimamo wao mechi ya tarehe 21 haitakuwa na mashabiki, sisi Simba Sports Club tumejaribu kuwashawishi mashabiki waingie uwanjani na tungewasaidia kutangaza mchezo lakini wamekataa katakata.”
“Mchezo ambao mashabiki wetu mtaingia utapigwa Jumapili Oktoba 25, 2026 saa 10:00 jioni. Baada ya kutupa taarifa ya kukataa mashabiki baadae tukapata taarifa kwamba wanafanya mpango wa chinichini kuwe na mashabiki, sasa msimamo wetu kama Simba ni hatutakwenda uwanjani, sisi tutasubiri mechi ya tarehe 25.
Sisi tulitumia njia rasmi kuwasiliana nao wakakataa na wakatoa taarifa na CAF, sasa wanapita nyuma ya pazia kutafuta mifumo ya kuuza tiketi na hatujui wanashirikiana na nani. Wakiuza tiketi sisi mashabiki hatutanunua.”
“Roho zinatuuma sababu huu ndio wakati sana wa kuiona Simba yetu lakini sababu wameleta ugaigai na sisi tunawaletea ugaigai, tarehe 21 tutavumilia tutakwenda kuiona Simba yetu tarehe 25. Lakini hawa mabwana walikataa mashabiki? sababu ni mashabiki wetu Wanasimba, wanafahamu kama wangeruhusu mashabiki kuja uwanjani pamoja na kuwa wenyeji wa mchezo lakini wangekuwa wageni kwa sababu 100% ya mashabiki ambao wangekuja uwanjani ni wetu.”
“Baada ya FC 15 de Agosto kukataa mashabiki, mdhamini wetu mkuu kampuni ya Betway Tanzania akasema wanangu msikae kivyonge, nitafanya jambo kwa ajili ya Simba Sports Club. Ametuandalia screen kubwa ambayo atafungwa hapahapa katika viwanja vya Mwenye2-1 na tutakutana hapa kuangalia mchezo huo mwanzo mwisho.”
“Tuna kila sababu mashabiki wa Simba kujipongeza, ukiona mtu anakuzia kwenda kwenye jambo lake maana yake anajua nguvu ambayo upo nayo, anajua madhara ambayo unaweza kuisababisha.”- Semaji Ahmed Ally
Chanzo: Simba Sports Club