kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Viongozi wetu wakuu nchini ni wapenzi wa waziwazi wa simba na yanga. Mfano, Mheshimiwa Makamu wa Rais na waziri wa fedha ni shabiki lialia wa Yanga, Waziri Mkuu na Spika ni mashabiki lialia wa simba. Viongozi hawa wote walikuwa kwenye birthday na uzinduzi wa Kitabu cha Mzee Mwinyi siku na wakati uleule mechi ya Simba na Yanga ilipaswa kuanza SAA 11 jioni.
Bila shaka nao kama watanzania wangependa kulishudia lile pambano la watani wa jadi live. Na bahati mbaya Uzinduzi wa Kitabu kile usingeweza kusogezwa nyuma wala mbele ili kupisha mechi hiyo kwasababu uzinduzi ulikuwa umefungamanishwa na birthday ya mzee ambayo haiwezi kusogezwa.
Hivi kwa akili za kibinadamu inawezekanaje MTU kama mh. Mwigulu, Ndugai na Waziri Mkuu waikose mechi kama hii hivihivi eti kwasababu tunazindua Kitabu cha Mzee Nzasa.
Je, kwa mazingira kama hayo hakuna uhusiano kati ya mechi kuahilishwa na sherehe ya birthday ya Mzee wetu Mwinyi? Kama upo uhusiano ni nani alaumie, TFF, Kamati ya ligi, kamati ya Massa 72, Yanga, Simba, Wizara ya michezo, Mzee Mwinyi, Rais, au viongozi wa siasa wanaoshabikia Simba na Yanga?
Kwa namna yoyote ile hakuna MTU yeyote ambae yuko juu ya mpira wa simba na Yanga nchini, busara itumike na iwe fundisho kwa siku zijazo kupanga kitu chochote sambamba na Mechi ya simba au na Yanga.
Ndio maana hata ufanyeje sababu hasa ya mechi kusogezwa kutoka SAA 11 kwenda 1 usiku haitatolewa milele.
Itafutwe siku ingine mechi ichezwe tusitafute mchawi.