Mechi ya Simba ns Azam, Mwamuzi hakunyima penati pande zote?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Mimi ni Yanga na niwe wazi tu siuungi mkono maamuzi mabovu ya Waamuzi na huwa najiuliza ni hatua gani huchukuliwa kwa waamuzi wanaofanya maamuzi mabovu?

Binafsi ndio maana siku zote mimi huwa naunga mkono mstumizi ya VAR ingawa kuna watu wanapinga halafu watu hao hao wanalalamika maamuzi mabovu ya waamuzi kwenye ligi yetu.

Tukirudi kwenye mada, mechi ya juzi ya Simba na Azam, hakukuwa na maamuzi mabovu ya pande zote kunyimwa penalti?

Kama maamuzi yale uliyaunga mkono, basi huna haki ya kuhoji wala kulalamiikia maamuzi ya Mechi ya leo baina ya Yanga na Geita Gold.

Ukipenda boga, penda na ua lake.

TFF huu ujinga katika soka letu ufike mwisho. Inaboa sana.

Kama waamuzi hawana viwango, wapigwe chini.

Tumechoka.
 
Tukirudi kwenye mada, mechi ya juzi ya Simba na Azam hakukuwa na maamuzi mabovu ya pande zote kunyimwa penalti?

Kama maamuzi yake uliyaunga mkono, basi huna haki ya kuhoji wala kulalamiikia maamuzi ya Mechi ya leo baina ya Yanga na Geita Gold.

Ukipenda boga, penda na ua lake.

TFF huu ujinga katika soka letu ufike mwisho. Inaboa sana.

Kama waamuzi hawana viwango, wapigwe chini.

Tumechoka.
Nilkuwa nakuona mpagania haki kweli,kipindi cha harakati za chadema,kumbe wapi,yanga I moyoni mwako sana,unakwama wapi kusema leo mmebebwa,unakuja na vijimfano vya mchongo ili uhalalishe uovu
 
Umesoma na kuelewa nilichoandika au unakurupuka tu?
 
Mmetoa hela kwa mwamuzi acha kupindisha maneno
 
Bora hapo aliona amekosea kutompa Azam akaja akabalance na Simba ilipokosea. So wote walinyimwaaa loose loose situation 😆 😆
 
Bora hapo aliona amekosea kutompa Azam akaja akabalance na Simba ilipokosea. So wote walinyimwaaa loose loose situation [emoji38] [emoji38]
Mpira unachezeshwa kwa kufuata sheria 17 za soka na sio kubalansi mchezo kama unavyosema wewe
 
Kolo kapoteana. Alitegemea geita ambebee mzigo lkn kashindwa. Sasa bwana kolo, mbina ww ulibebwa mechi ya Prisons? Alaf kingine bwana kolo, Mayele alivinyimwa goli vs mtibwa sugar mechi ya maamuzi hatima ya mfungaji bora, hukushangilia ww?

Kingine bwana kolo last seasons mechi dhid ya Prisons na Mbeya kwanza hukushinda kwa mbrleko ww?

Yanga zile point ulizozibeba kiwizi dhidi ya Prisons pale mbeya kazibeba pale ccm kirumba.
 
Nilkuwa nakuona mpagania haki kweli,kipindi cha harakati za chadema,kumbe wapi,yanga I moyoni mwako sana,unakwama wapi kusema leo mmebebwa,unakuja na vijimfano vya mchongo ili uhalalishe uovu
Ndugu kwa huyo utapoteza MB zako buure

Huwa anailaumu CCM kila leo kumbe nae anatamani apate nafasi waliyonayo CCM ili anufaike pia

Ndio maana huwa nasema wengi wanaoikosoa CCM huwa wanaona donge tu wenzao kuwa jikoni sio kama wanachukizwa na mapungufu yaliyopo.
 
Mimi ni Yanga na niwe wazi tu siuungi mkono maamuzi mabovu ya Waamuzi na huwa najiuliza ni hatua gani huchukuliwa kwa waamuzi wanaofanya maamuzi mabovu?

Binafsi ndio maana siku zote mimi huwa naunga mkono mstumizi ya VAR ingawa kuna watu wanapinga halafu watu hao hao wanalalamika maamuzi mabovu ya waamuzi kwenye ligi yetu.

Tukirudi kwenye mada, mechi ya juzi ya Simba na Azam, hakukuwa na maamuzi mabovu ya pande zote kunyimwa penalti?

Kama maamuzi yale uliyaunga mkono, basi huna haki ya kuhoji wala kulalamiikia maamuzi ya Mechi ya leo baina ya Yanga na Geita Gold.

Ukipenda boga, penda na ua lake.

TFF huu ujinga katika soka letu ufike mwisho. Inaboa sana.

Kama waamuzi hawana viwango, wapigwe chini.

Tumechoka.
Ni bora unyime penalty ya mashaka ijapo inaweza kuwa kweli kuliko kutoa penalty huna uhakika.

Mwamuzi wa leo alikuwa na matukio mengi ya kupendelea yanga.
 
Ndugu kwa huyo utapoteza MB zako buure

Huwa anailaumu CCM kila leo kumbe nae anatamani apate nafasi waliyonayo CCM ili anufaike pia

Ndio maana huwa nasema wengi wanaoikosoa CCM huwa wanaona donge tu wenzao kuwa jikoni sio kama wanachukizwa na mapungufu yaliyopo.
Huyu jamaa nilkuwa namwaminia sana,kumbe nae akipewa fursa atatupiga tu,yana anashindwa kuwakemea wanautopolo wenzake
 
Makolo wakibebwa refa ana mapungufu ya kibinadamu
Ile mechi ya yanga na makolo wanapewa penalti nje ya box walishangalia
Kuna msimu mechi inafika dk 90 wanaongezewa zaidi ya dakika 10 wakifunga goli ndo mpira unaisha kipindi chote tulivumilia
 
Back
Top Bottom