Mechi ya taifa stars vs Tunisia 17/11/2020 kuchezwa saa 20:00Pm, karibu kwa updates

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,102
Reaction score
1,919
Kuna mkanganyiko wa baadhi ya websites kuhusu mechi ya leo kuhusu muda utakapochezwa mchezo wa taifa stars na Tunisia, wengine wameandika saa nne usiku wengine saa mbili usiku, uhalisia ni mechi itaanza saa mbili kamili usiku, karibuni kwa updates za uhakika
====
Kama una mb za kutosha, fuatilia kupitia hiyo link
 
Azam wenyewe wanaoonesha hiyo mechi wamesema mechi itaanza saa 4, acha kudanganya umma.
 
Fuatilia vizuri asee.Hadi TFF wenyewe washaweka saa nne
 
Kama unatumia mfumo wa masaa 24 huwa hakuna AM na PM. Kwa Military clock ingepaswa kuwa 20:00 ama 20:00hrs.
 
Tanzania itashuka katika dimba la Benjamin Mkapa leo katika mchezo wa marudio wa kuwania kufuzu #AFCON2022 dhidi ya Tunisia. Mchezo huo utakaoanza saa 4:00 usiku ni muhimu kwa Taifa Stars kuweza kufufua matumaini ya kushiriki fainali hizo zitakazopigwa nchini Cameroon. https://t.co/LZg8eycuQn
 
Kama vipi Leo Staz ivae tena jezi za Njano kwa kuwa zinasaidia timu ifungwe magoli machache.
Zile jezi za Blue za nyumbani hazina Bahati, hazivutii na kubwa zaidi jezi zilisababisha Timu iitwe kichwa cha Mwendawazimu.
 
Hayo masaa ya usiku ni friendly sana kwa hao Waarabu.Hii game ingekuwa ipigwe saa 8 au 9 mchana hapo ningekuwa na matumaini, ila sasa HATUNA CHETU HAPO.
 
Hatuna uwezo was kuchezesha mechi saa nne usiku, mechi nisaa mbili, tembelea @CAF online
 
Wakizungumza na waandishi wa habari jana, viongozi wa BMT na TFF wakiwa na wajumbe wa Kamati ya Ushindi walithibitisha kuwa mchezo kati ya Taifa Stars na Tunisia utachezwa kuanzia saa 4.00 za usiku, kwa mujibu wa maelekezo ya CAF yanayozingatia Haki za Matangazo ya TV ( TV rights ).
Sasa kama kuna mtu ana maelezo tofauti basi atuambie ni mamlaka ipi iliyobadilisha muda?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…