Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Kariakoo Derby kupigwa leo Jumamosi ya Mei 8 2021 katika mfululizo wa michuano ya Vodacom Premier League (VPL), ambapo Mabingwa wa Nchi Mnyama Mkali Simba SC, anapepetana na Mwananchi Yanga SC kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jiji Dar es salaam.
Katika mchezo ambao utavuta hisia za mashabiki kutoka kila upande, unatarajiwa kuwa mkali sana kwa muda wote wa dakika 90 huku kila timu ikihitaji alama tatu muhimu kuweza kujiweka sawa kwenye msimamo wa (VPL).
Simba SC, mpaka kufikia wa leo anaongoza Ligi Kuu Tanzania kwa alama 61 akiwa ameshuka dimbani kwa michezo 25 na amefunga mabao 58 na kuruhusu mabao 10.
Yanga SC inashika nafasi ya pili kwa alama 57 akiwa ameshuka dimbani kwa michezo 27 na amefunga mabao 41 na kuruhusu mabao 17.
Kocha Msaidizi wa Simba SC Suleiman Matola, ameahida burudani pamoja na ushindi katika mchezo huo huku akiongeza kuwa;
"Inabidi tushinde mchezo ili tuwe na nafasi nzuri ya kutetea ubingwa. Na hakuna mchezaji yeyote ambaye tunaweza tutamkosa kwenye mchezo wa kesho (leo).
Tunataka tukawape watu burudani, lazima tukacheze mchezo ambao tumeuzoea kucheza, na siku zote timu inayomiliki mpira ina nafasi kubwa ya kupata matokeo ya ushindi tunawaambia mashabiki wetu waje kutushangilia, hatutawaangusha". alisema Kocha Msaidizi Matola.
Naye Kocha wa Yanga Nasreddine Al Nabi, amesema kuwa "Simba SC ni timu nzuri lakini ina mapungufu yake, tunaiheshimu lakini hatuihofii.
Maandalizi ya mechi ni yale yale kama michezo mingine tofauti ni uchezaji, tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tumejiandaa kushinda
Nampongeza Kocha Didier Gomez kwa kuifanya Simba SC kucheza soka safi ndani hata Ligi ya Mabingwa Afrika na hii inatoa taswira nzuri kwa soka la Tanzania". alisema Kocha Nabi.
Hakuna namna ila dakika 90 za Derby hii ya Kariakoo zitaamua ndani ya Dimba la Mkapa.
Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1: 00 Usiku.
KWANI WAO WANASEMAJE?..GUMZO HAPO NDIPO..USIKOSE UKASIMULIWA.
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana.
====
Yanga waingiza timu uwanjani
SAA 10:58 jioni kikosi cha Yanga kimeingia uwanjani na jezi za mchezo kwa maaa ya flana za njano na bukta nyeusi kwa lengo la kuanza mchezo.
Wachezaji 11 ambao ni Metacha Mnata, Adeyum Saleh, Shomari Kibwana, Bakari Mwamnyeto, Abdallah Shaibu, Mukoko Tonombe, Feisal Salum, Tuisila Kisinda, Said Ntibazonkiza, Yacouba Sogne na Michael Sarpong waliingia katika eneo la kuchezea huku wengine wakikaa benchi.
Baada ya kuingia walikaa upande mmoja wa uwanja kimafungu mafungu wakipiga stori huku wakiwasubiri wapinzani wao Simba na waamuzi wafike uwanjani hapo.
Ikumbukwe kuwa dakika chache baada ya tukio hilo tayari wachezaji wa Yanga walikuwa wameingia uwanjani hapo wakiwa na jezi za kupashia na kuondoka baada ya muda mfupi.
Si waamuzi wala wenyeji Simba walioonekana uwanjani hapo kwa wakati huo.
Credit: Ramadhan Elias
=====
UPDATES : 1830HRS
UPDATE: Bodi ya Ligi Tanzania imetangaza kuahirisha mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga iliyokuwa ichezwe leo
- Yanga waliingia na kutoka Uwanjani kutokana na mchezo huo uliokuwa uchezwe saa 11:00 jioni kupelekwa mbele saa 1:00 usiku
#JFSports