Mechi ya Yanga FC Vs TP Mazembe - Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Bora wewe umemuuliza maana mi nikadhani timu yake haijacheza leo wakati ndo hao hao wamekubali kamoja japo kwa shida
hahahahaaaa mkuu shida tu, kama simba ndio alicheza uwanjani
 
Atamtambia nani, maneno mengi kama kasuku lakini vitendo hakuna maana hawa raia wanaolilia kujenga uwanja bondeni kwenye mafuriko ambako NEMC wamekataza hawana sera
basi ajifunze kufunga mdomo wake maana akianza kutapika mpaka anahara aise!
 
hahahahaaaa mkuu shida tu, kama simba ndio alicheza uwanjani
Mi ngoja niwasemee kwa muda:
ee unajua wakimataifa hoi tumefungwa japo kwa tabu sana maana tumewapiga vyenga weee lakini tulipojisahau kidogo tu wakafumua kwa bahati mbaya ila yatakwisha
 
Soka safi kwa kipigo ila niliweka wazi YANGA siwapendiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Hii inaitwa ringa tena...au unaimba " amerudi analia eeh..... Anatia huruma....mtanzania mwenzetu ametutoa kimasomaso
Ulimwengu hana huruma...Anawapiga watu chenga mpaka wanaomba msamaha😀😀😀😀
 
Team ya Dar Young Africans leo imefanikiwa kuchapwa bao Moja na TP Ya TP Mazembe katika uwanja wa Taifa Dsm.

Katika Pambano hilo Yanga walicheza Kabumbu safi sana ambalo haljawah kuonekana Dunian lakin bahat tu haikiwa yao baada ya mipira yao mingi kugonga mwamba na kutoka sentimita chache sana.

Kiukwel team hii IMEENDELEA KUFA KIUME katika mechi zake za hivi karibuni.
 
KwaYanga ninayoifahamu mimi ile ya pale mitaa ya Jangwani na twiga,bila refarii kutoa ushirikiano wa kugawa' mi redi kadi' isiyokuwa na mpangilio na 'mipenati tata' basi matokeo huwa hivi...!huwa inabaki tulicheza mpira mwingi japo takwimu za mechi zinakataa(Ball possessions 47% Yanga,53% TP Mazembe). Kobe akiwa juu ya mti lazima ujiulize amefikaje?
 

Hapo kwenye RED ndio huwa panaturudisha nyuma wabongo, dunia ipi mkuu??
 
Yanga inapaishwa na mashabiki lakini timu kama timu ni hapa ndani tu lakini nje ya mipaka ya nchi yetu ni wakuolewa tu.
 
Dah umenikumbusha ule msemo maarufu kwamba kufungwa tumefungwa lakini chenga tumewala...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…