Wakuu wote wa JamiiForums,
Leo jumanne jioni ya saa 10 katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam itapigwa mechi kati ya Yanga ya Tanzania na TP Mazembe ya Congo DRC!
Ni mechi ya kimataifa, Kombe la Shirikisho la Mpira barani Afrika CAF! Tayari Yanga ina rekodi ya kufungwa katika mechi ya kwanza na MO Bejaia ya nchini Aljeria.
Mechi ya leo Yanga imejigamba kushinda na imefanya mkakati wa kuingiza wanachama wake bure ili kutia nguvu. Tutakuwa Live hapa JF kuwaletea matukio yote kabla na baada ya mechi.
Pia Azam TV na Super Sport itakuwa live. Asubuhi na mapema mashabiki wa Yanga na wapenda kabumbu kwa ujumla wameanza kumiminika Taifa kushuhudia kipute
Kikosi kamili cha Yanga leo
Leo mungu asaidie Thomas Ulimwengu aiongoze vyema timu yake itoke na ushindi mnono TaifaLeo mungu asaidie Yanga ishinde
Kweli kabisa Mkuu.Tuwe wazalendo,tumsaport mtanzania mwenzetu Thomas ulimwengu
Hata kama wataenda milion 3 mmeruhusiwa kuingia 40,000 tu , wengine wote watarudishwa , na mpaka muda huu taarifa zinasema mabomu yameanza kurushwa , unajua ni kwanini ? Watu ni wengi kuliko idadi inayotakiwa .Sifahamu Elimu yako. Nilichojifunza kupitia post hii, wewe ni mtu mwenye mawazo finyu sana. Ule uwanja unajazwa na watu 60,000 tu. Idadi hiyo ni asilimia ngapi ya wakazi wa Dar es Salaam? Chukulia kuwa population ya Dar es Salaam kwa sasa ni kama 4.1million, watu 60,000 ni kama 1.46%, kati ya hawa ni nini probability ya kuwa mashabiki wa Yanga? Je, mashabiki wa timu nyingine ni kiasi gani? Na wale ambao ni wapenzi wa mpira tu, si wapenzi wa Yanga ni kiasi gani? Endapo maswali haya hayana majibu ya kisayansi, je uko wapi uhalali wa kudai kuwa walioingia uwanjani wote ni mashabiki wa Yanga? Uko wapi sasa uhalali wa kudai kuwa mashabiki wa Yanga ni jobless?
Poor mikia fc, mmeanza kulalama mapema, sijui itakuwaje saa 12 baada ya TP Mazembe kulala 2-0.
Wengine madoctor wanafanya kazi part time usiku hadi asubuhiBasi tuseme ni walinzi wakati wa usiku
Bila shaka wee ni Banyamulenge,mmekwisha leo hamna pakutokea.Kweli kabisa Mkuu.
Tuwe wazalendo,tumsaport mtanzania mwenzetu Thomas ulimwengu
Ukishasema part time, maana yake ameajiriwa mahali fulani for full time. Sasa uwanjani saa 12 hadi 2 usiku kuna daktari gani anaweza kufanya hicho? Hao hawana kazi, serikali ichukulie hiyo kama sample ya utathmini wa ajiraWengine madoctor wanafanya kazi part time usiku hadi asubuhi
Good question , ni hivi , siku zote mimi na mke wangu tumejiwekea utaratibu wa kufanya Jogging mapema sana asubuhi , kutoka kwetu Tandika Mwembe Yanga hadi uhasibu kupitia Uwanja wa Taifa , nadhani sasa umeelewa kwanini nimewaona hao mashabiki wa Yanga wasio na kazi za kufanya .We mwenyewe upo kundi hilo hilo umejuaje yote hayo kqma haupo eneo la tukio?
Ukija Taifa, ukijua huipendi Yanga,tafadhali funga mdomo wako kwa karatasi kama wale jamaa wa UKAWA mjengoni. Usikosee kushangilia wageni, nitakwenda jela kwa ajili yako. Sina utani, ugenini tunanyanyasika sana ,tena mbele ya askari wao.
mleta mada alivyomnafiki wala hajui mechi ya kwanza Yanga alicheza timu kutoka Nchi gani go yanga gooo hii ni timu ya WANANCHI
Nakushukuru sana kwa huruma yako kwa Watanzania wenzetu wasio na kazi .Ukishasema part time, maana yake ameajiriwa mahali fulani fo full time. Sasa uwanjani saa 12 hadi 2 usiku kuna daktari gani anaweza kufanya hicho? Hao hawana kazi, serikali ichukulie hiyo kama sample ya utathmini wa ajira
hiv hawa jamaa wana mkataba wa kudumu?lINK YA kustream live
Link ya KU-STREAM LIVE Yanga Vs TP Mazembe
مشاهدة مباراة يانغ أفريكانز ومازيمبي بث مباشر بتاريخ 28-06-2016 كأس الإتحاد الأفريقي
Huna lolote wivu wa kike unakusumbua,wee ni wa matopen itu, tulia nyumbani kwako uangalie kwenye tv,waache wasio na kazi wakaangalie live,wee inakuumiza nini ?hawana kazi sawa una msaada gani katika hilo kwao?waache wafanye linalowafurahisha nafsi zao,halafu ni muongo sana wewe kwa taarifa yako uwanja umeshajaa na milango imeshafungwa sasa hayo mabomu wanapigwa kina nani? tembelea blog za kimichezo za saleh jembe na bin zubeiry uone kinachoendelea na kukaa kwenye kisimu chako na kutunga uongo usio na tija.Hata kama wataenda milion 3 mmeruhusiwa kuingia 40,000 tu , wengine wote watarudishwa , na mpaka muda huu taarifa zinasema mabomu yameanza kurushwa , unajua ni kwanini ? Watu ni wengi kuliko idadi inayotakiwa .
Utaratibu wakuingia ukoje mkuu