Mechi ya Yanga na Simba ikiamuliwa kurudiwa litakuwa ni kashfa kubwa zaidi ya Upangaji wa Matokeo kuwahi kutokea katika Soka Afrika na duniani

Mechi ya Yanga na Simba ikiamuliwa kurudiwa litakuwa ni kashfa kubwa zaidi ya Upangaji wa Matokeo kuwahi kutokea katika Soka Afrika na duniani

Dadi Barnea

Member
Joined
Nov 30, 2024
Posts
40
Reaction score
33
Ikiwa TFF na Bodi ya Ligi wataamua Mechi ya Yanga ni Simba ichezwe tena, hilo litakuwa ni tukio kubwa la Match fixing kuwahi kutokea katika Soka la Afrika na duniani.

Na kwa kuwa inaonekana ni hujuma ambayo ilipangwa mapema(premeditated) kwamba Yanga wagomee mechi ya marudiano ili Simba wapewe points 3 za bure na Yanga wanyang’anywe points 15, hili llitakuwa ni tukio la kwanza la Uchafu na Ufisadi usiomithilika unaohusisha chombo kinachosimamia Soka nchini na Klabu wanayojaribu kuibeba. Itakuwa ni kiwango cha juu kabisa cha Ufisadi na kukosa haya.

Kwa kuwa habari za chini chini zinasema namna pekee ya kuokoa mechi hiyo kuchezwa tena ni kumwalika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au wa Zanzibar kuwa Mgeni Rasmi wa Mechi hiyo, wito wangu kwa viongozi hawa ni kugoma hadhi yao kutumika kama dodoki kusafisha uchafu huu.

Soma Pia: Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba

Ni vizuri vyombo vya Usalama vya nchi vikatimiza wajibu wao ipasavyo kumshauri Rais, au kiongozi yeyote ambaye TFF na Bodi ya Ligi watataka kumtumia kama dodoki wasikubali kutumika katika Uchafuu huuu. Karia aachwe alinywe alilolikoroga maana keshazoea uhuni wa hapa na pale.

Mwalimu Nyerere alikwishasema mtu akizoea kula nyama ya mtu hataacha kula. Karia amefanya mambo mengi ya kipuuzi ambayo yote ni kama huwa anatoka scot free hivi, not this time.

Match fixing ni uhalifu mkubwa katika soka. Karia na watu wake sasa wakati umefika wawajibike.
 
Back
Top Bottom