Mechi ya Yanga na Zamaleki imeshamalizika

Mechi ya Yanga na Zamaleki imeshamalizika

kibaigwa finest

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2026
Posts
411
Reaction score
445
Shabiki wa timu ya Zamalek ya Misri baada ya kuona orodha ya timu walizopangwa nazo kwenye kundi lao, ametoa maoni yake kuhusu kundi hilo.

"Tutacheza dhidi ya MC Alger kutoka Algeria, Yanga Africans, na Club Africain kutoka Tunisia. Alhamdulillah (Namshukuru Mungu), semeni Alhamdulillah, Insha'Allah (Mungu akipenda) mambo yatakuwa sawa, na msimu huu utakuwa mgumu sana. Mambo yataenda kama yatakavyoenda, lakini sisi ndio mabingwa wa michuano hii."

"Sisi ndio bora zaidi kwenye mashindano haya, hakuna utani hapa."

"Sawa basi, twende taratibu; vaeni nguo zenu kwa sababu tuna mechi yetu baada ya masaa mawili. Kuhusu utabiri wangu, tutaifunga Club Africain, tutatoka sare dhidi ya MC Alger, na kwa vyovyote vile, mechi dhidi ya Yanga Africans imeshamalizika (tayari tumeshinda)."
 
Kiasili waarabu hawawezi kudhibiti jazba na mbaya zaidi wana tabia ya kwenda uwanjani na maatokeo yao mfukoni. Mambo yakiwa tofauti wanaanzisha vurugu. Wale jamaa wa beiulzdad walivyopigwa chuma nne kwa mkapa, kocha na mchezaji wake walitaka kuzipiga uwanjani
 
Asubiri maajabu ya mpira, Yanga na Club African wanafuzu Robo Fainali kundi B.
 
Back
Top Bottom