Manara karudia Yale Yale ambayo alikuwa anafanya Nugaz, uwanja unajazwa na Mashabiki wa Simba alafu yeye anajipa pongezi Kwa kuhamasisha kujaza uwanja
Kwa hii miaka ya karibuni, game za derby zote haijarishi Simba ni mwenyeji au Yanga ni mwenyeji, bali mashabiki wa Simba watakuwa wengi tu na sijui Yanga waga kwanini hawajitokezi Kwa wingi kama kwenye siku ya wananchi
Imefkia hatua viongozi wa Yanga kama Senzo na muhamasishaji Manara wanapost picha za uongo ili kuaminisha watu kwamba mechi ya Juzi Yanga walikuwa wengi kuliko Simba, ni aibu kwa viongozi kujaribu kupotosha kwani kasumba ya Yanga kutoingia wengi kwenye derby haijaanza Leo
Senzo na Manara wanatumia picha za siku ya wananchi ya mwaka Jana kuaminisha watu kwamba walijaza uwanja kitu ambacho sio kweli, wao wajikite katika kuboresha team na washabiki watakuja Tu wenyewe kama ilipofkia Kwa mashabiki wa Simba
Simba hawajafanya promo yoyote ili mashabiki waende uwanjani hadi Bumbuli akalalamika kuwa Simba Wana roho mbaya hawataki kuipromo derby kwa sababu wanajua Yanga watapata pesa nyingi
na of course ni kweli Simba walikuwa wanajua Tu mashabiki wao ndio watajaza uwanja ata kama wao sio wenyejei na ndio kilichotokea, robo Tatu ya uwanja ilikuwa ni mashabiki wa simba, kwahiyo hii game kuongoza Kwa mapato sio ajabu maana huo ni mwendelezo wa kila msimu Kwa Yanga kunufaika na Mashabiki wa Simba
Kwahiyo kama Manara alikuaga anadhania mashabiki wa Simba wanajaa uwanjani Kwa ajili yake alikuwa anapotea, pamoja na kufanya tour kila Media ila alichoambulia ni number ile ile ya siku zote Kwa mashabiki wa Yanga, Kwa lugha rahisi zaidi ni kwamba katika swala la mashabiki kuingia uwanjani hajapunguza chochote kwa Simba na wala hajaongeza chochote kwa Yanga
View attachment 2208266
View attachment 2208266