Mechi ya YANGA yaingiza mapato zaidi kuliko mechi za Simba, hata zile za CAF

Mechi ya YANGA yaingiza mapato zaidi kuliko mechi za Simba, hata zile za CAF

Nasikitika kukuita mtoa Uzi BOYA..yaani takwimu za Manara ndiyo unazitumia hapa
 
Wala sio uongo ni kweli aliongoza ila ni msimu uliopita Tu na sio kawaida yao, na aliongoza Kwa sababu ya mashabiki wa Simba kuingia wengi kwenye derby zote 2, Yani haijarishi Yanga ni mwenyeji au mgeni bali mashabiki wa Simba ndio huwa wengi

Sasa leo hii Manara anahusisha kuingia mashabiki wao wengi na wao kuingiza mapato mengi, Hadi anapost picha za siku ya wananchi mwaka Jana ili Tu aaminishe watu kwamba Yanga walikuwa wengi katika Derby ya Juzi kuliko Simba

Ukiangalia namba katika Derby ya Juzi ni almost robo 3 ya uwanja walikuwa ni mashabiki wa Simba ilhali Yanga ndio mwenyeji, alafu leo kiongozi kama Senzo anapost picha za mwanachi day ni aibu nayeye kufata mkumbo wa ndugu yetu Manara

inaonekana ata viongozi wa Yanga na wao wanapenda kuona mashabiki wa Yanga wawe wanaingia wengi kwenye derby ili ionekane tofauti na miaka ingine, ila ndo hivo tena sijui mashabiki wa Yanga waga wanaogopa nini kwenda wengi kwenye derby na ata kama wao ndio wapo kwenye form nzuri ila waga hawaendi wengi
Kwa iyo mashabiki wa Simba wanajaa kwenye derby tu? kumbuka katika derby 2... Moja mapato yalikuwa ni ya Simba...Ina maana mechi nyingine za Yanga na timu nyingine, mapato ya Yanga yaliizidi ya Simba...Au na mechi zote za Yanga wanaoenda ni mashabiki wa Simba?
 
Manara karudia Yale Yale ambayo alikuwa anafanya Nugaz, uwanja unajazwa na Mashabiki wa Simba alafu yeye anajipa pongezi Kwa kuhamasisha kujaza uwanja

Kwa hii miaka ya karibuni, game za derby zote haijarishi Simba ni mwenyeji au Yanga ni mwenyeji, bali mashabiki wa Simba watakuwa wengi tu na sijui Yanga waga kwanini hawajitokezi Kwa wingi kama kwenye siku ya wananchi

Imefkia hatua viongozi wa Yanga kama Senzo na muhamasishaji Manara wanapost picha za uongo ili kuaminisha watu kwamba mechi ya Juzi Yanga walikuwa wengi kuliko Simba, ni aibu kwa viongozi kujaribu kupotosha kwani kasumba ya Yanga kutoingia wengi kwenye derby haijaanza Leo

Senzo na Manara wanatumia picha za siku ya wananchi ya mwaka Jana kuaminisha watu kwamba walijaza uwanja kitu ambacho sio kweli, wao wajikite katika kuboresha team na washabiki watakuja Tu wenyewe kama ilipofkia Kwa mashabiki wa Simba

Simba hawajafanya promo yoyote ili mashabiki waende uwanjani hadi Bumbuli akalalamika kuwa Simba Wana roho mbaya hawataki kuipromo derby kwa sababu wanajua Yanga watapata pesa nyingi

na of course ni kweli Simba walikuwa wanajua Tu mashabiki wao ndio watajaza uwanja ata kama wao sio wenyejei na ndio kilichotokea, robo Tatu ya uwanja ilikuwa ni mashabiki wa simba, kwahiyo hii game kuongoza Kwa mapato sio ajabu maana huo ni mwendelezo wa kila msimu Kwa Yanga kunufaika na Mashabiki wa Simba

Kwahiyo kama Manara alikuaga anadhania mashabiki wa Simba wanajaa uwanjani Kwa ajili yake alikuwa anapotea, pamoja na kufanya tour kila Media ila alichoambulia ni number ile ile ya siku zote Kwa mashabiki wa Yanga, Kwa lugha rahisi zaidi ni kwamba katika swala la mashabiki kuingia uwanjani hajapunguza chochote kwa Simba na wala hajaongeza chochote kwa Yanga

View attachment 2208266

View attachment 2208266
Alafu kitu kingine kama hujui... Hata kwenye magazeti..Yanga ikishinda, magazeti yananunuliwa sana..tofauti na Simba inaposhinda... Hapo ndio ujue nguvu ya Yanga ilipo
 
Alafu kitu kingine kama hujui... Hata kwenye magazeti..Yanga ikishinda, magazeti yananunuliwa sana..tofauti na Simba inaposhinda... Hapo ndio ujue nguvu ya Yanga ilipo
Makolo....Wanabisha....
 
Back
Top Bottom