Mechi za CAF za kufuatiliwa Week-end hii

Mechi za CAF za kufuatiliwa Week-end hii

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Week-end hii ndipo mizunguko ya michezo ya CAF inakamilika. Kutakuwa ni michezo 16 lakini ya muhimu kufutaila ni hii hapa chini kwa vile mingine itakuwa ni ya kumailisha ratiba tu.

CAF-CL

  1. Yanga Vs MC Alger: Mechi hii itaamua ni nani kati ya washindani ataingia robo finali na itakuwa ya mvutano sana
  2. Al-Ahly Vs Orlando Pirates: Wote Orlando Pirates na Al Ahly wameshafuzu robo fainali, lakini mechi hii ndiyo itakayoamua ni nani ataongoza kundi lao.
  3. Mamelodi Vs AS Far Rabat: Wote wameshafuzu kuingia robo fainali, lakini mechi hii ndiyo itakayoamua nani anakuwa mshindi wa kwanza kwenye kundi lao
  4. Raja Cansablanca vs Maniema Union: Hawa wote ni kiama wameshatolewa, na wanapigania nafasi ya tatu, lakini Raja Cansablanca anaweza kuitazama nafasi ya pili iwapo Mamelodi atafungwa na AS FAR Rabat. Kwa hiyo michezo yote miwili ya kundi B ni ya kufuatiliwa kwa karibu sana.

CAF Confederation
  1. Simba SC vs CS Constantine: Hawa wote wamshafuzu robo fainali wanapigani kuongoza kundi lao, kwa hiyo watashindana sana.
  2. Al-Masry Vs Black Bulls: Hawa wanagombania nafasi ya pili, kwa hiyo itakuwa ni mechi ya nguvu sana kwani kila mmoja atautaka ushindi.
  3. USM Alger vs Jarraf: Hawa pia wanagombania nafasi ya kuongoza kundi
  4. ASEC Mimosa Vs Orapa united: Hawa wangomania nafasi ya tatu kwenye kundi lao, ila iwapo Jaraafu ikufungwa halafu ASEC Mimosa ikashinda basi ngoma inaweza pia kuishindansiah ASEC Momosa dhid ta Jarraf.
  5. Zamalek vs Enyimba: Huu ni mchezo unaoonekana kama wa low energy ila una implications kadhaa. Iwapo Enyimba itaifunga Zamalek halafu Black Bulls ikaifunga El-Masry basi Enyimba itachukua nafasi ya pili kwenye kundi. Kwa hiyo michezo yote miwili kwenye kundi D ni ya kufuatilia kwa karibu sana
 
Orlando Pirates kajipata msimu huu hacheki na yoyote. Hilo kundi lao gumu lakini katoboa. Mamelodi yapo waliyumbayumba lakini bado wamo. Yanga nao sio kinyonge mechi mbili za mwanzo hawakua na point saivi mechi ya 5 wana point 7. SIwezi kumuombea kheri mwarabu hata siku moja afungwe tu.
 
Back
Top Bottom