Mechi za CAF za vilabu afrika Azam TV anapewa bure (FTA) je, kwanini wao wanarusha kwenye pay TV kama Azamsport hd1 na si channel za bure?

Munch wa annabelletz47

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2019
Posts
1,885
Reaction score
3,227
Je huu sio utapeli kwa watanzania? kama unapewa haki ya kurusha matangazo bure kwanini we uuze? Tunaomba ufafanuzi kwenye hili kabla mechi za timu za Tanzania za leo. Pia TCRA, TFF, FCC na wizara ya sanaa na michezo mpo wapi? kwani hamlijui hili swala na je nyie wachambuzi hamlioni hili pia? au mpaka mama aongee mwenyewe?
 
Unaweza kubishana kwa kizungu?
 
Acha tulipie tuangalie vizuri. Hao TBC HOPELESS
 
Bora umegusia
 
Leo utume email CAF kwa ushahidi wa channel ya AzamSports HD 1, tuone majibu yatakuwaje!
 
Kwani makubaliano ya Azam na anayempa yakoje?

Anakatazwa kuuza au hakatazwi?

Hicho ndicho kitu muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…