Mechi za kimataifa ni ngumu sana kwa timu iliyozoea kuhonga na kubebwa

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Nimekuwa nikisema kuwa matumizi ya pesa kwenye mpira kufanya ushawishi kwa wachezaji wa timu pinzani, kwa waamuzi na wachambuzi wa mchongo, matokeo yake yataonekana mechi za kimataifa.

Katika mechi hizi hakuna cha wazee waliopigania uhuru wala sijui mashabiki wa ukweli, Ni uwezo wa wachezaji na akili. Mechi hizi siyo za kukamia kama inavyofanyika kwenye ligi yetu.

Kama mnataka kushinda punguzeni matumizi ya vipesa vya kuhonga honga na kutumia wazee kuwatia kiwewe makochaa wa timu pinzani wafanye mabadiliko ya kijinga.

Wekezeni kwenye uwanja kuliko kuwekeza nje ya uwanja na propaganda nyingi.

Wape salaam.
 
Na hii itawacost sana utopolo kuamini wapo vizuri kumbe wananunua mechi mfano leo lile goli la mayele la ofside ingekuwa bongo wangepewa kifupi yanga hamna kitu ila ujanja wa ligi yetu kununua mechi ndio kunawafanya waonekane bora angalia hata mwaka jana simba ndani inaonekana mbovu ila ilifika robo shirikisho wakati yanga mwaka jana nzuri hata makundi hawakufika unajifunza nini hapo
 
Kuna muda utafika kivuli cha JF kitaacha kuwa kichaka cha watu kujificha na kuzusha habari za uongo zisizokua na mantiki.

Muda utafika tu. Wajinga kama mleta mleta mada wataelimishwa na kuachana na haya mambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanajivunia kuwa unbeaten wakati kiuhalisia ni unbeaten wa mchongo maana kuna maamuzi mabovu mengi tu kutoka Kwa hawa marefa wetu wa mchongo yamewaokoa wasipate vipigo, mfano dhidi ya Namungo.

Hii ligi ya ndani ni kuwezesha kupata tiketi tu ya kimataifa lakini sio ya kujiona wewe unatimu Bora kisa tu umechukua ubingwa wa hii ligi ya ndani.
 
timu yetu haikuwa na bahati na baada ya kufunga wachezaji walijisahau na kuamini mechi imeisha. kwao watapigika tu mpira wao wa kuvizia hamna kitu possession hawana!

kesho baada ya mechi wanasimba msitukimbie mtakula nne bila
 
timu yetu haikuwa na bahati na baada ya kufunga wachezaji walijisahau na kuamini mechi imeisha. kwao watapigika tu mpira wao wa kuvizia hamna kitu possession hawana!

kesho baada ya mechi wanasimba msitukimbie mtakula nne bila
ahahahahah
 
Ingekuwa mechi na Kagera Sugar goli la offside la Meyele ingekuwa kamba. Refa anajifanya kama hajaona vile kusingizia makosa ya Kibinadamu.

Anyway tukutane Sudani
 
Ingekuwa mechi na Kagera Sugar goli la offside la Meyele ingekuwa kamba. Refa anajifanya kama hajaona vile kusingizia makosa ya Kibinadamu.

Anyway tukutane Sudani
Simba mara ngapi wanafunga magoli haramu na yanakubaliwa??
 
Wanalowazana eti wana timu nzuri wakati ni mbovu tu

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Napenda waendelee kujifariji hivyo hivyo Unbeaten na mazagazaga mengine ili waendelee kudumaa hapo hapo walipo.

Si toka Karne ya 21 haijawahi kucheza makundi, basi wacha tu waendelee na ngojera tu yaani..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…