Mechi za kirafiki kabla ya Kombe la dunia

Mechi za kirafiki kabla ya Kombe la dunia

Siempre Hechos

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2016
Posts
1,157
Reaction score
1,413
Wana JF, habarini wakuu!

Jana nilipata nafasi ya kuangalia mechi za kirafiki lakini mechi mbili zilinivutia sana, mechi kati ya German vs Brazil na pia Spain vs Argentina. Lakini kwa mtazamo wangu wa haraka haraka na uelewa wangu mdogo wa mpira, nimeona kama timu zilizofanaya vibaya katika kombe la dunia lililopita hasa Spain na Brazili zimebadilika na zimeonesha uhai katika michuano ya kombe la dunia lijalo. Brazil alishinda 1-0, Spain alishinda 6-1.

Katika kikosi cha Argentina Messi hakucheza na kama angecheza swali nalojiuliza ni kwamba
1. Spain wangeshinda kwa idadi hiyo kubwa ya magori?
2. Argentina wangeshinda?
3. Spain wangeshinda lakini si kwa idadi kubwa hiyo ya magori?
Au Spain ni mbabe kwa Argentina?, Au Spain karudi kwenye kiwango chake? au ni mbwembwe tu za Spain kwenye majaribio?

NOTE: Isco akifunga har-trick.

Karibuni kwa mitazamo yenu wale wapenzi wa soka.

 
Back
Top Bottom