Mechi za makundi CACL na CAFCCL kufanyika uwanja wa Uhuru stadium

Mechi za makundi CACL na CAFCCL kufanyika uwanja wa Uhuru stadium

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema ana matumaini makubwa kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litaidhinisha Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kutumika kwa mechi za hatua ya makundi ya mashindano ya klabu barani Afrika.

Akijibu maswali ya mwandishi wa habari za michezo wa TBC, Hussein Shafii, Karia amesema anaendelea na jitihada za kuhakikisha uwanja huo unakidhi vigezo vya CAF kwa wakati.

Amesema Simba na Yanga, zinazoshiriki hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, pamoja na Azam FC na Singida Black Stars, zinazoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika, zinatarajiwa kutumia uwanja huo kuanzia wiki mbili zijazo, endapo utapata idhini ya CAF.

 
Nafikiri ndio uwanja unao ongoza kwa marekebisho na bila kutumika, hadi kuna muda nawaza ni kichaka cha watu kupigia pesa?
Halafu bado uwanja upo kizamani halafu baada ya marekebisho hakuna Jipya kama Vilevile tu
 
Back
Top Bottom