Mechi za mchana ni hatari kwa afya ya wachezaji kutokana na joto kuwa juu

Mechi za mchana ni hatari kwa afya ya wachezaji kutokana na joto kuwa juu

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
4,445
Reaction score
4,707
Wadau mlio wengi mtakubaliana nami juu ya maada hapo juu.Tumeshuhudia vilabu vyetu vikicheza mpira Mchana wa saa 8 huku hali ya hewa ikiwa ya joto sana karibia nyuzi joto 34 kwa miji ya Dar,Tanga na Morogoro.Joto la kiasi hicho ni hatari kwa Wachezaji wetu ukizingatia mchezo wa mpira unatumia nguvu nyingi.Wachezaji wetu wanachoka,wanatoka jasho jingi hivyo kupelekea kupungukiwa na maji mengi wakati wa mchezo. Madhara ya hali hiyo ni kuishiwa maji mwilini,Mapigo ya moyo kuongezeka na Moyo kusimama ghafla na kupelekea vifo kwa Wachezaji wakiwa Viwanjani.Tunaishauri Bodi ya Ligi na TFF waliangalie hili kabla halijatokea.Kama ni sehemu zenye Baridi halina shida ila mikoa yenye kiwango cha juu cha joto ni hatari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom