Mechi za mwisho VPL,Vita ya ubingwa na kushuka daraja

*************************************
YANGA BINGWA MSIMU WA 2016/2017
*************************************
FULL TIME | Simba 2 - 1 Mwadui
FULL TIME | Mbao FC 1 vs 0 Yanga
FULL TIME | Majimaji 2 vs 1 MBC
FULL TIME | Mtibwa 3 vs 1 Toto
FULL TIME | Ndanda 2 vs 0 Jkt Ruvu.
FULL TIME | Azam 0-1 Kagera Sugar
FULL TIME | Stand 1-0 Ruvu Shooting

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA

DK 89 Ndemla anapiga kichwa safi kabisa lakini Kado anaokoa vizuri na mwisho inakuwa kona isiyo na manufaa

DK 85, shambulizi kali la Mwadui lakini mwamuzi anasema walikuwa wameishaotea

Dk 80 sasa, Simba wametawala zaidi katikati na Mwadui FC wamerudi nyuma kabisa wakionekana kufanya mashambulizi ya kushitukiza huku Simba wakiwa wameshindwa kuipenya ngome ya MWadui

Dk 75, Kichuya anaachia mkwaju mkali kabisa hapa lakini anapiga juuuuu

Dk 70, nafasi nzuri kwa Simba, lakini Athanas anang'ang'ania mpira bila sababu, Cholo anaokoa vizuri kabisa

SUB 67, Pastory Athanas anaingia upande wa Simba kuchukua nafasi ya Ajibu

Dk 66, Muzamiru anaachia mkwaju mkali lakini Kado anafanya kazi ya ziada, anaokoa inakuwa kona. Yuko chini anatibiwa

DK 65 Simba wanapata kona ya sita, Kichuya anapiga kona fupi kwa Bukungu , Juuko anaachia mkwaju mkali lakini, kipa Shabani Kado yuko makini

SUB DK 61 Salim Kabunda anaingia kuchukua nafasi ya Hassan Kabunda

Dk 56, Simba wametawala zaidi katikati ya uwanja lakini hakuna mashambulizi makali

SUB Dk 53, anaingia Mwinyi Kazimoto na kuchukua nafasi ya Laudit Mavugo

Dk 48, Miraji anaachia mkwaju lakini Agyei anaonekana yuko makini

Dk 47, Simba inafanya kona ya kwanza kipindi cha pili, inachongwa lakini haina madhara

Dk 46 Mwadui FC wanaonekana kujibu mashambulizi lakini bado hakuna utulivu

Dk 45, Simba wanaonekana kuanza kwa kasi zaidi, hii inaonekana wanataka mabao ya haraka

SUB Dk 45 Ndemla ndani ya nyumba, anachukua nafasi ya Liuzio

HALF TIME | Simba 2 - 1 Mwadui
HALF TIME | Mtibwa 1-1 Toto African
HALF TIME | Ndanda 1-0 JKT Ruvu
HALF TIME | Majimaji 1-0 Mbeya City
HALF TIME | Prisons 0-0 Lyon
HALF TIME | Azam 0-1 Kagera Sugar
HALF TIME | Stand 1-0 Ruvu Shooting

MAPUMZIKO
-Chollo anaachia mkwaju mkali hapa lakini Agyei anadaka vizuri kabisa

DAKIKA 2 ZA NYONGEZA

Dk 45, Mwadui wanaonekana kucharuka zaidi na kugongeana vizri katikati ya uwanja

GOOOOOOOOO Dk 44, anaachia mkwaju mkali baada ya kupokea pasi nzuri ya Kabunda na kuandika bao safi

Dk 42 Nonga anajaribu shuti kali kabisa lakini Agyei anadaka vizuri kabisa

Dk 39, Shuti la Mavugo linamgonga Mngeveke na kuwa kona, inachongwa hapa na kuondoshwa na Awadhi Juma

Dk 38 mpira unaendelea tena na Simba wanaonekana kuzidi kutawala

Dk 37, mpira umesimama, waamuzi wanajadili jambo hapa

Dk 32, nafasi nyingine nzuri kwa Simba lakini Kichuya anashindwa kuwa makini anashindwa kufunga

Dk 31 sasa, Simba wanaonekana kuutawala mpira kwa sasa hasa katika eneo la katikati ya uwanja

Dk 28, Kabunda anazunguka vizuri na kuachia mkwaju mkali lakini hakulenga lango

GOOOOOOOOOOO Dk 25, Ajibu anaiandikia Simba bao la pili baada kugongeana vizuri na Liuzio anampa pasi nzuri kabisa

Dk 23 Awadhi Juma anaachia mkwaju mkali kabisa lakini goal kick

Dk 21, Mavugo anaachia mkwaju mkali, kipa wa Mwadui anapangua na kuwa kona. Inachongwa hapa haina manufaa

GOOOOOOOOOOOO Dk 18 Kichuya anafunga mkwaju wa penalti na kuiandikia Simba bao la kwanza

PENAAAAAAAAAAT....Dk 16 Simba wanapata penalti baada ya kipa Shabani kumgonga Kichuya, wachezaji Mwadui wanamzonga mwamuzi

Dk 14, Mavugo anatoa pasi safi kwa Kichuya akiwa katika nafasi nzuri anajaribu kufunga, unaokolewa na kuwa kona. Inachongwa hapa lakini haina madhara

Dk 13, Mwadui wanajichanganya na Mavugo anajaribu lakini kipa anaokoa

Dk 12 sasa, MWadui FC ndiyo wanaoonekana kuutawala zaidi mpira hasa katika eneo la katikati na Simba wako nyuma wakifanya mashambulizi ya kushitukiza

Dk 8 Ajibu anatoa pasi safi kabisa kwa Mavugo lakini Mavugo yeye na kipa, anachelewa

Dk 8, Mwadui wanafanya shambulizi kali kupitia awadhi Juma na kupata kona, inachongwa lakini wanaokoa

Dk 2, Simba wanajibu mashambulizi lakini krosi nzuri ya Ajibu haina mwenyewe, goal kick

Dk 1, Mwadui ndiyo wanaonekana kuanza kwa kasi kama wamepania kupata bao la mapema

Credit: Saleh Jembe
 
Hivi kuna wa kuizuia Yanga leo isitwae ubingwa kwa mara ya 27.?
Simba katwaa mara 18 tu.
Aisee , hapa kuna tofauti kubwa kati ya kaka na dada.
 
Simba 2 - Mwadui 0.

GOOOOOOOOOOO Dk 25, Ajibu anaiandikia Simba bao la pili baada kugongeana vizuri na Liuzio anampa pasi nzuri kabisa
Dk 23 Awadhi Juma anaachia mkwaju mkali kabisa lakini goal kick
Dk 21, Mavugo anaachia mkwaju mkali, kipa wa Mwadui anapangua na kuwa kona. Inachongwa hapa haina manufaa
GOOOOOOOOOOOO Dk 18 Kichuya anafunga mkwaju wa penalti na kuiandikia Simba bao la kwanza
PENAAAAAAAAAAT....Dk 16 Simba wanapata penalti baada ya kipa Shabani kumgonga Kichuya, wachezaji Mwadui wanamzonga mwamuzi
Dk 14, Mavugo anatoa pasi safi kwa Kichuya akiwa katika nafasi nzuri anajaribu kufunga, unaokolewa na kuwa kona. Inachongwa hapa lakini haina madhara
Dk 13, Mwadui wanajichanganya na Mavugo anajaribu lakini kipa anaokoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…