Mechi za mwisho VPL,Vita ya ubingwa na kushuka daraja

Mechi za mwisho VPL,Vita ya ubingwa na kushuka daraja

Klabu ya Simba imegoma kuchukua zawadi ya mshindi wa pili mara baada ya mchezo wake wa mwisho wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mwadui FC.

Licha ya ushindi wa Simba wa magoli 2-1 na kufikisha alama 68 sawa na Yanga ambayo imepoteza mchezo wake wa mwisho kwa kufungwa 1-0 na Mbao FC, bado Simba imejikuta ikimaliza katika nafasi ya pili kutokana na tofauti ya wastani wa magoli.

Baada ya mchezo wa Simba vs Mwadui kumalizika kwenye uwabja wa taifa, MC alitangaza kwamba timu ya Simba itapewa zawadi kulingana na nafasi waliyomaliza (ya pili) huku Yanga wakiwa wametwaa ubingwa wa VPL 2016/17.

Jambo la kustaajabisha ni pale viongozi na wachezaji kuonekana kutojali zawadi hiyo, walielekea vyumba vya kubadilishia nguo mara baada ya mchezo.

Walisubiriwa kwa dakika kadhaa lakini hawakutokea, walipoulizwa baadhi ya viongozi walijibu kwamba wachezaji wanabadili jezi walizochezea na kuvaa nguo maalum kwa ajili ya kwenda kupokea zawadi hizo.

Kadiri muda ulivyozidi kuyoyoma bado Simba waliendelea kusalia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na mara kadhaa wachezaji na viongozi walitoka na kurudi tena vyumbani.

Waandishi wa habari waliokuwepo uwanjani kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo walianza kuondoka mmoja baada ya mwingine na kuwaacha wachezaji wa Simba wakiwa bado hawajatoka ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo.
Ningekuwa mm ni simba ningejitoa kwenye ligi you kwani miaka mingi sjapata kombe.
 
Yaani kuongoza ligi kwa tofauti ya point 8 tena kwa kipindi kirefu adi kudondokea nafasi ya 2 mwishoni mwa ligi???
Hapana kuna sehemu simba imekosea either kwenye safi ya uongozi au kwa wachezaji, tena bila kurekebisha hili mwakani yatakua yaleyale!
 
Najiuliza hii jeuri ya TFF kugawa zawadi wakati kuna rufaa FIFA inatoka wapi? Hata kama wanadhani rufaa haina mashiko wanashindwa kuheshimu mfumo wa kutoa haki unaotambulika kimataifa? Ningewashangaa viongozi wa simba kama wabgekubali kupokea hizo zawadi
 
Mi nashauri hilo kombe wapewe Simba wakae nalo wakati wanasubiri maamuzi ya Fifa, ikionekana Simba wameshinda rufaa basi watabki nalo, na ikitokea wameshindwa basi walipeleke yanga na wao wchukue zawadi yao ya mshindi wa pili
 
Najiuliza hii jeuri ya TFF kugawa zawadi wakati kuna rufaa FIFA inatoka wapi? Hata kama wanadhani rufaa haina mashiko wanashindwa kuheshimu mfumo wa kutoa haki unaotambulika kimataifa? Ningewashangaa viongozi wa simba kama wabgekubali kupokea hizo zawadi
Uliambiwa ligi imesimama? Acheni hizo. Forgery waliyofanya baadhi ya wajumbe kuhalalisha kadi isiokuwepo itawapa ban ya maisha. Subiri muone, Kulialia FC!!
 
Yote haya kayasababisha Kagera kumpiga simba 2....... Kagera Mungu anawaona
 
Haina sababu ya kupokea zawadi za mpora kombe Malinzi wa yanga. Kamati ya uendeshaji wa ligi ilishatoa point 3. Malinzi kapora na inshomile wenzake leo simba watapokeaje zawadi ya mtu aliyewapora? Tuwe wakweli unatoaje kombe ambalo tayari limekatiwa rufaa.
 
Simba wajikite kwenye maandalizi dhidi ya mbao. Maana ubao umemchoma chura mara mbili bila aibu. Haya mambo ya vita na inshomile wawaachie kina kaburu na Aveva.
 
Back
Top Bottom