Mechi za Simba, Azam zinahitaji kumulikwa

Mechi za Simba, Azam zinahitaji kumulikwa

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,025
Reaction score
1,270
HABARI za michezo katika siku za hivi karibuni zimekuwa zikipambwa zaidi na habari kuhusu nafasi ya Yanga kutwaa taji la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa msimamo wa ligi na hatua ambayo ligi imefikia ni wazi Yanga ndiyo timu ambayo inasubiriwa kukabidhiwa rasmi taji hilo.
Na upo uwezekano mkubwa wa Yanga kumaliza kazi hiyo leo Jumatatu itakapoumana na Polisi Moro, mechi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga inayoshika usukani wa ligi ikishinda leo itafikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote na kutokana na mwenendo wa Polisi Moro ni wazi kwamba Yanga inapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi.
Huo ni ukweli ambao hata timu za Azam na Simba ambazo zinazoifukuzia Yanga kwa karibu zinaujua kwamba Yanga inaweza kumaliza kazi leo hasa kwa kuzingatia udhaifu wa Polisi Moro katika ligi.
Wakati Yanga ikiwa na hesabu zinazoeleweka katika mbio za kutwaa ubingwa, kazi bado ipo kwa timu za Azam inayoshika nafasi ya pili na Simba inayoshika nafasi ya tatu.
Timu hizo kwa sasa ni kama zipo katika vita ya kuwania nafasi ya pili ambayo inaipa nafasi timu kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Azam ina pointi 45 wakati Simba ina pointi 41 na timu zote hizo kila moja imebakisha mechi tatu kabla ya kumalizika kwa ligi.
Ni wazi mechi hizo tatu kimahesabu zinaweza kuishusha Azam na kuipandisha Simba au kuiacha Azam ilipo nafasi ya pili na Simba ya tatu.Kwa maana nyingine ni vita ya pointi tisa kabla ya kumalizika kwa ligi, ingawa Azam ina nafasi nzuri hasa itakaposhinda mechi yake ijayo. Bado hofu ya mambo ya rushwa katika mechi zilizobaki haiwezi kuwekwa kando au kupuuzwa kwa namna yoyote.
Kwa kuliona hilo ndiyo maana tunachukua nafasi hii kuwakumbusha wenye dhamana ya usimamizi wa soka yaani Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwa makini na mechi hizi na si vibaya kuitumia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) katika hilo.
Tunasisitiza jambo hilo kwa sababu kwa hatua ambayo ligi imefikia suala la timu kuhongwa au baadhi ya wachezaji au waamuzi si la kupuuzia.
Kwa hatua ambayo ligi imefikia, zipo baadhi ya timu ambazo hazina cha kupoteza, zitaendelea kubaki katika ligi na pia baadhi ya wachezaji wanaweza kurubuniwa kiurahisi kwa sababu ama wanataka kuachana na timu hizo au wanajua hawana cha kupoteza.

Kibaya zaidi ni kwamba hujuma za aina hii, huwa haziishii kwa wachezaji tu, zipo habari kuwa hata baadhi ya viongozi hutumika katika kuhujumu timu zao hasa wakati huu ambao ligi inaelekea ukingoni.
Ni vyema mambo kama haya yasidharauliwe, yafanyiwe kazi ili ligi imalizike salama na washindi wa kweli wapatikane ili soka liweze kuendelea.
Bado tunaikumbuka kauli ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi kutokuwa na msamaha na rushwa katika soka lakini tungependa kumkumbusha kwamba kauli hiyo ni jambo moja na ufuatiliaji ni jambo la pili.
Ni muhimu aweke mashushushu na ikiwezekana asisite kuwatumia Takukuru.

Source :Mechi za Simba, Azam zinahitaji kumulikwa - Soka - mwanaspoti.co.tz
 
Huyu mwandishi nawadhani hawatendei haki timu za Simba na Azamu.Hajaweza elezea kwanini mechi ya timu hizi mbili zimulikwe ukizingatia kwamba tofauti ya point 4 iliyopo kati ya hizi timu mbili ni kubwa.Hivi katika mechi zilizosalia timu zilizo na point juu ya 30 zina chakupoteza kama watauza mechi? Je kuna ushahidi wowote kwamba timu za Azam na Simba ni mabingwa wa kununua mechi na wachezaji? Hivi katika mechi ya Yanga na polisi hakuna hofu ya Yanga au Polisi kununua wachezaji wa wachezaji wa timu pinzani? Yamkini na mimi nimefikiria vibaya ILA hayo ndiyo maoni yangu.
 
Kama sikosei Simba anamzidi Azam mechi moja

Ni kweli Mkuu, Azam wanaizidi Simba point 4 huku wakiwa na mechi moja mkononi. Hata kama Azam itapoteza mechi hiyo na kuwa na idadi sawa ya mechi na Simba, bado pengo la point 4 liko palepale. Simba wana kazi ya ziada kupata nafasi ya pili.
Wangekuwa na mechi na point sawa, labda mechi kati yao ingemua nani ashike nafasi ya pili. Mbaya zaidi kwa Simba, mechi ya mwisho ya Azan wanacheza na Yanga. Endapo Yanga itakuwa imenyakua ubingwa kwa kuifunga polisi, ni dhahiri hiyo mechi ya mwisho kwao itakuwa haina maana zaidi ya kulinda heshima. Wanaweza kuwapa nafasi wachezaji ambao hawakupata sana nafasi kwenye ligi.
 
Labda kwataarifa nenda kawaambie yanga atuhongwi ila.matokeo yatakuwa hivi
azam 3:yanga 2


kamamlikaza mwakajana azam achukue ubingwa tunakazua mwakahuu azam awewa pili. Hiyopelekanatakukuru kabsa
 
Sikuhiyo utawajuawachezaji wayanga wote resevu nakunawakutuuliza
 
Simba lazima achukue nafasi ya pili

Ulazima wa simba kuchukua nafasi ya pili unatoka wapi!!!!!
Kumbuka azam wana game tatu mkononi na katika game hizo 3 wanahitaji point 3 tu ili kufikisha point 48 ambazo haziwez kufikiwa na timu ya simba.
Sasa labda nikuulize, hiv unadhani azam wanaweza kupoteza game zote hizo 3 bila kupata point 3???!
 
Back
Top Bottom