Media Stations kuvunjiana vipindi kwa kuibiana watangazaji wakuu, hii imekaaje!

Media Stations kuvunjiana vipindi kwa kuibiana watangazaji wakuu, hii imekaaje!

Kwangu naona imekaa poa. Ina faida kwa watangazaji wenyewe ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamika kuwa na maslahi duni kwenye fani hiyo.

Baada ya Efm kuwavunjia Wasafi Tv & Fm kipindi cha Sunday Worship kwa kuwachukua Lilian Mwasha & Masanja, sasa Wasafi nao wamefanya REVENGE kwa kuwachukua watangazaji nyota wa kipindi cha Joto la Asubuhi, Maulid Kitenge & Gerald Hando.

Ngoja tusubiri Efm watakuja na "CounterAttack" ipi.

View attachment 2592847

View attachment 2592849

View attachment 2592850

View attachment 2592851
Hapa ndio penyewe, husikubali unyonge
 
Kitenge amezid aiseee Ila hivo vipindi vyao
Vyote wasaf na efm hata waungane nadhan watabak kua chin ya sports extra
Hakuna wakupindua hawa jamaa
Duh... mbona unaongelea vipindi vyenye maudhui tofauti.. ungesema Power Break fast.
 
Duh... mbona unaongelea vipindi vyenye maudhui tofauti.. ungesema Power Break fast.
Mm nimesema Kwa vipindi vya michezo
Sports arena, sports HQ, sports extra

Lakin hata hapa kwenye good morning,joto la asubuh, power break fast

Bado mawingu anawapiga tatu bila nje ndan
 
Mm nimesema Kwa vipindi vya michezo
Sports arena, sports HQ, sports extra

Lakin hata hapa kwenye good morning,joto la asubuh, power break fast

Bado mawingu anawapiga tatu bila nje ndan
Hapo mi naikubali sports arena ya wasafi, hawa jamaa hawana story binafsi nyingi kama hao wengine. Sports hq ndo bure kabisa full story zao.

Hivyo morning vingi ni story zao tu na kuongea na kujazia nyama vitu wasivyojua kiundani. Kidogo clouds wana desturi ya kuita wataalam.
 
Maisha hayattabiriki kabisa
Watu wazima professionals wanasherehekea kuajiriwa na mdogo wao aliefeli form four kutoka Tandale....
Life is really unpredictable

Bro, wengi wa wanaotengeneza ajira siyo doctorates, wengi wao kama kasoma sana wanaishia Masters, ila Form IV, VI na wengi Darasa la Saba ndo watoa ajira wengi!!

Na sababu kubwa wao wanatake risk kubwa bila kuwaza sana, na ndo wanaotoboa kwenye mafanikio na kutoa ajira kwa vipanga wengi waliokuwa wanasoma nao!!

Ila pia sasa imagine kila mtu aseme sitaki kuajiriwa nataka kujiajiri mwenyewe!! Hiyo fujo itakuwaje? Kuna kitakachofanyika kweli!!

Naamini ipo hivyo tu kuwa wawepo wanaojiri na wanaojiriwa ila balance ya maisha iweze kwenda mbele. Tofauti na hapo dunia itakuwa uwanja wa fujo!!
 
Ñi sawa tu na kwenye soka kunyanga'ana wachezaji. Tusijisahaulishe Azam media ilivyoibomoa Star TV kwa kuwachukua Ahmed Ally, Inona na Baruani
 
Maisha hayattabiriki kabisa
Watu wazima professionals wanasherehekea kuajiriwa na mdogo wao aliefeli form four kutoka Tandale....
Life is really unpredictable
Mkuu maisha tukisema tuyachukulie kwa staili hiyo,tutaishia kuumia tu bila kuyaenjoy hata kidogo.Tuwaache wakae wanapoona wanastaili haijalishi iwe kwa form four aliefeli toka Tandale au mwenye phd wa osterbay.
 
Ñi sawa tu na kwenye soka kunyanga'ana wachezaji. Tusijisahaulishe Azam media ilivyoibomoa Star TV kwa kuwachukua Ahmed Ally, Inona na Baruani
Hawakuwachukua hao tu. Listi ni hii
1. BARUAN MUHUZA
2. IVONA KAMUNTU
3. AHMED ALLY
RAYMOND NYAMWIHULA
4. RAHAB FRED
5. STEVE MOYO MCHONGI
6. HASSAN MVULA

Ikafika muda ukiwa unatazama azam ni kama unatazama startv
 
Back
Top Bottom