Medical diagnostic centre

Medical diagnostic centre

faby

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2011
Posts
2,214
Reaction score
767
Heshima zenu wakuu, nina mpango wa kufungua Medical diagnostic centre hapa jijini dar es salaam,ambapo vipimo nazo fikiria kuweka ni ultrasound, EEG, ECG, laboratory ya upimaji damu na dentist.ushauri wenu na mawazo yenu yanahitajika kwa sana, ie;gharama za hizo machines,proper location,madaktari nitawapataje etc. asanteni. CC ZeMarcopolo
 
Last edited by a moderator:
Wazo zuri sana.

Kwa hivi sasa maeneo ambayo yana opportunity zaidi ni Chang'ombe, Temeke, Mbagala na Segerea.

In the future eneo perspective ni Kibada, ingawa kwa sasa bado halichangamka sawasawa.

Maeneo hayo niliyotaja yana uwekezaji mdogo wa sekta ya afya.

Kutokana na madaktari wengi walioanzisha huduma za afya kuwa na uhusiano na Muhimbili, na wengi wao wanafanya kazi pia Muhimbili, huduma nyingi binafsi wanazotoa zinapatikana maeneo yasiyo mbali sana na Muhimbili kama Upanga, Kariakoo, Kinondoni etc.

Wewe ninakushauri uende nje ya hapo. Mahitaji yako jiji zima.

Kutokana na sheria ya nchi yetu utalazimika kutafuta daktari au madaktari ambao watasajiriwa kama wasimamizi wa sehemu hiyo inayotoa huduma.

Ukishafanya maamuzi ya Wilaya unayotaka kufungua kituo, fiko ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo ili upatiwe maelezo ya vigezo unavyotakiwa kukidhi. Wao ndio watakaokagua eneo lako na kukuwekea sign kwenye fomu utakayoipeleka Wizarani kuomba kibali cha kufungua kituo. Kwahiyo ni muhimu kuwashirikisha katika hatua za awali.

Vilevile unaweza kuwasiliana na uongozi wa chama cha madaktari Tanzania kupitia doctorsmat@gmail.com ukiwaomba wakuunganishe na madaktari wenye interest ya ushirikiano katika huduma unayopanga kutoa. Nijuavyo ni kwamba MAT bado hawana utaratibu huo, lakini email yako itakuwa chachu ya kuanzishwa kwake. Kila jambo lina mwanzo wake.

Bottomline: Mahitaji katika huduma za afya ni makubwa. Ukipata wataalam wazuri na ukazingatia maadili ya uwekezaji katika sekta ya afya, una kila sababu ya kufanikiwa. Go for it...
 
naomba MUNGU ufanikiwe kwenye shughuli zako.asante kwa kunitia moyo,i will update u in the near future ZeMarcopolo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom