Megastructures mlizozipinga zimeibadili taswira ya Tanzania, mlikurupuka kumkosoa Rais Magufuli

Megastructures mlizozipinga zimeibadili taswira ya Tanzania, mlikurupuka kumkosoa Rais Magufuli

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Wapinzani wa Tanzania wanakasumba mbaya sana. Wao kila jambo ni kukosoa tu.

Wakiona serikali inajenga shule, hospital, barabara au stendi ya mabasi wao ni kukosoa tu.

Nimeshuhudia mabadiliko makubwa sana kwenye miji yetu tangu JPM awe rais. Naweka baadhi ya mifano. Nilishuhudia mkoa wa Singida ukipata stendi mpya ya kisasa iliyogharaimu bil 12 +.

Pia tumeshuhudia stendi mpya ya kisasa jijini Dodoma na soko kubwa la kisasa la Ayubu Ndugai. Stendi mpya ya mabasi ya Magufuli ni ya kutiliwa mfano. Maana ni zaidi ya Johanesburg Park Station.

Wapinzani tokea JPM aingie madarakani mlikuwa mnakosoa na kumdhihaki kuwa ni mzee wa kupenda Megastructures. Je, sasa hamuoni zilivyobadili taswira ya taifa letu? Hamuoni kuwa ni kaendeleo makubwa na miundo mbinu ya kisasa ambayo itaongeza mapato kwa taifa?

My take; Tusipende kukosoa kila kitu,hata mradi wa JNHPP ukikamilika itakuwa ni Megastructure inayotusaidia.
 
Megastructure sio za mtu inabidi zijengwe kwa kuzingatia long term plans na city master plan inasemaje na mahitaji kwa wakati husika, unaweza ukajenga kitu kikawa a white elephant.

Kwahio ujenzi wote mkubwa lazima uzingatie michango ya wadau / wataalamu na wahusika wa pande zote sio mmoja tu kuamua najenga hiki au kile. Mpaka sasa kama nchi tungekuwa tuna long term na short term plans za nini kinajengwa na wapi na kwa faida ya nani Tangia Enzi za Mwinyi hawa viongozi kazi yao ni kutekeleza tu.

Sio kiongozi atakayekuja sababu anatoka Gamboshi aamue kwamba mji uhamie Gamboshi (kabla hajamaliza muda wake tupate kiongozi wa Ukara) na yeye aamue ujenzi wake, Kwa precedence hii tunaweza tukawa na nchi ya unfinished projects.
 
Hiyo stand mpya ya Mbezi is exaggerated ni ya kawaida sana hasa ukilinganisha na za nchi nyingine, sijaona upekee kihivyo.
 
"DOLA YA NYUKI"

Nyuki daima huwa anawaza kutengeneza asali tu!

Maisha ni zaidi ya asali.😃😃😁😁🤣🤣
 
Kwa hiyo zinapo ibadili hiyo taswira ya Tanzania ndiyo kusema na maisha ya wananchi yameboreka, au? Mataga mna akili za ajabu sana.
GDP ya tanzania mpaka january imefika $70B, just $19 billion less to lead the whole east africa, kwahio kwa haraka haraka tuseme ule mradi wa mafuta wa uganda + sgr will be enough to throw us mpaka atleast $94B, this is all you need to know kuhusu swla la maisha kuboreka hilo ni swala la jitihada za mwananchi mwenyewe! tayar infrastructure umewekewa! kama unafanya kilimo kusafirisha mzigo mpaka dar kwa treni haizidi 8K, kwa basi inafika mpaka 20K, kazi imebaki kwako sasa.
 
GDP ya tanzania mpaka january imefika $70B, just $19 billion less to lead the whole east africa, kwahio kwa haraka haraka tuseme ule mradi wa mafuta wa uganda + sgr will be enough to throw us mpaka atleast $94B, this is all you need to know kuhusu swla la maisha kuboreka hilo ni swala la jitihada za mwananchi mwenyewe! tayar infrastructure umewekewa! kama unafanya kilimo kusafirisha mzigo mpaka dar kwa treni haizidi 8K, kwa basi inafika mpaka 20K, kazi imebaki kwako sasa
Mko vizuri sana kwenye taarifa za kwenye makaratasi! Ila ukija kwenye maisha halisi ya Watanzania, mambo ni tofauti kabisa.

Mna mkakati wowote ule wa kuboresha kilimo awamu hii? Mna mkakati wa dhati wa kuboresha mazingira ya kufanya biashara?

Mna mkakati wowote ule wa kupunguza tatizo la ajira na pia kuboresha maisha ya wafanyakazi? Kote huko majibu yamekaa kisiasa na kinadharia zaidi! Kubali tu, Raus wako kipenzi ni failure!!
 
Tuliza akili kwanza kabla ya kuandika kwanza hiyo mambo ya stendi na Masoko sio mawazo ya JPM yeye kaukuta mpango ambao tayari unatekelezwa wenyewe wanaita ULGSP and DMDP mfano kwa mkoa wa Njombe Stendi ilianza 2013 na ulikua mradi ulioenda sambamba na soko,Msavu morogoro ni miradi iliyoanza kutekelezwa awamu ya kwanza chini ya ufadhili wa World Bank.

Ukiondoa stendi masoko huenda yakawa kama machinga Complex ya Dar es Salaam yaliyokosa watumiaji na kubaki kama magofu bila sababu ya msingi kutokana na sera ya biashara popote ambayo imeruhusu watu kufanaya biashara na kumwaga bidhaa popote nje na masoko.Hivyo kujenga inaweza isiwe hoja hoja na faida yake.

Kama hoja ingekuwa ni kujenga hata Njombe unaweza kujenga international Airport huku ukiwa huna uhakika wa matumizi na ukaacha kujenga bararbara ambalo ndilo hitaji la msingi kwa ajili kurahisisha usafirishaji wa mazao.

Hivyo anayejenga na hoja na wanaokosoa wana hoja pia.
 
Mko vizuri sana kwenye taarifa za kwenye makaratasi! Ila ukija kwenye maisha halisi ya Watanzania, mambo ni tofauti kabisa.

Mna mkakati wowote ule wa kuboresha kilimo awamu hii? Mna mkakati wa dhati wa kuboresha mazingira ya kufanya biashara?

Mna mkakati wowote ule wa kupunguza tatizo la ajira na pia kuboresha maisha ya wafanyakazi? Kote huko majibu yamekaa kisiasa na kinadharia zaidi! Kubali tu, Raus wako kipenzi ni failure!!
Ki ukweli bado zinaweza kuwa zinaendeshwa kwa hasara na hili ukitaka kujua vizuri ni pale tunapoweza kuangalia ROI kwa kuangalia muda na rasilimali ilyotumika na tukachukulia kuwa huo ni mkopo wenye riba.

Bado jamii hainufaishi na uendeshaji au uwepo wa hizi stendi katika kuongeza kipato na hii inatokana na kuwa na viongozi wasio wabunifu katika kuwezesha kuongeza kipato - sioni sababu kwa stendi hizi zisiweze kufanya kazi masaa 24 angalau kwa kuwa na mabasi yatakayoenda mkoa mmoja kwa masaa 24 kwa pande nne mfano kituo cha Dodoma kiweze kuwa na safari zifuatazo kwa masaa ishirini na nne.
  1. Dodoma -morogoro
  2. dodoma Manyara
  3. Dodoma-singida
  4. Dodoma -Iringa
Na kila mkoa ikawa na root angalau za mkoa momoja kwa masaa 24 kiasi kwamba mtu akiwa anaenda arusha anauhakika akifika manyara atapata basi la Arusha na akiwa anaenda mbeya akifika Iringa atapata basi la kwenda mbeya.

Kwa kufanya hivi shughuli zingine zinaweza kuendelea kwa kadri ya mahitaji.

Haikai sawa eti unastend lakini huwezi kusafiri usiku hii haiko sawa.

Hili ni eneo moja lakini eneo lingine kunatakiwa kutengenezwe mazingira yanayovutia kumaliza baadhi ya mikusanyiko ya kijamii hukohuko stendi zikiwepo kumbi za sherehe na mikutano kiasi kwamba watu wakimaliza wanaondoka sambamba na kuweka hotel pamoja na lodge kwa wenye kipato cha kati na kawaida ili ikiwezekana akifanya shughuli zake aweze kulala stend na kuondoka.

Mighahawa mizuri na sehemu zenye bustani nzuri na michezo ya watoto inaweza kuongeza tija wakati watu wanasubiri wageni wanaweza kupoteza muda kwa kuwa maeneo hayo au mtu akavutiwa kwenda kutembea na familia badala ya kwenda bar.
 
1614584419669.png
 
Mmeua mzunguko wa biashara, mmeua kilimo, hakuna ajira! Mmeshindwa kuwapandisha vyeo wafanyakazi, nk. Hao wananchi watakao nufaika ni wananchi wa aina gani? Bodaboda na mama ntilie?
Manispaa ya ubungo itakuwa inapata bil 7+ kwa mwaka kupitia Magufuli bus terminal, unadhani hazitamsaidia mwananchi wa kawaida? Au unakaririshwa kukosoa tu?
 
Manispaa ya ubungo itakuwa inapata bil 7+ kwa mwaka kupitia Magufuli bus terminal, undhani hazitamsaidia mwananchi wa kawaida? Au unakaririshwa kukosoa tu?
Kwendraaa zako huko
 
Back
Top Bottom