mcshonde
Member
- Jul 15, 2022
- 66
- 154
Mehran Karimi Nasseri ni mwanaume ambaye ameishi ndani ya uwanja wa ndege kama nyumbani kwake kwa zaidi ya miaka 18. Serikali ya Iran ilimfukuza nchini bwana Nasseri bila kumpa pasi ya kusafiria (passport) wala viza kwa sababu alitoa kauli za kumpinga kiongozi mkuu wa nchi.
Alipotoka Iran alikwama kwenye uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa. Kwa kuwa hakuwa na nyaraka yoyote inayomtambulisha mamlaka ya uwanja wa ndege haikuweza kumruhusu aende popote na hata kumrudisha Iran ikawa ngumu kwani serikali ndiyo imemfukuza. Sheria kali za uhamiaji ulaya zikawa kikwazo kwani "ni mtu asiye na nchi" kwahiyo ilikuwa ni marufuku kwake kuvuka mlango na kutoka nje ya uwanja huo
Filamu ya The Terminal (2004) iliangazia uhalisia wa maisha yake na namna anavyotafuta pesa ya kujikimu hapo hapo uwanjani kuanzia Agosti 1988 hadi 2006: alikuwa anasaidia mafundi wanaofanya marekebisho mbalimbali, alisaidia kufanya usafi, alijenga urafiki na wasafiri waliokuwa wakimkuta kila wanapofika uwanjani hapo na wengine walimpa fedha kujikimu.
Alitumia muda huo pia kuandika historia ya maisha yake. Mwaka 2006 akawa dhaifu kiafya ndipo akapelekwa kwenye nyumba ya wazee aishi ingawa kila mara alikuwa anarudi uwanjani hapo kukaa kwani ameshazoea. Nasseri alifariki Novemba 2022 kwa mshtuko wa moyo.