Mei Mosi 2020: Rais Magufuli atuma salamu za siku ya wafanyakazi, asisitiza waendelee kufanya kazi na kujiepusha na Corona

Mei Mosi 2020: Rais Magufuli atuma salamu za siku ya wafanyakazi, asisitiza waendelee kufanya kazi na kujiepusha na Corona

Uongezewe maslahi wakati katika hali ya namna hii kuna kupunguzwa kazi, kukatwa mishahara maeneo mbalimbali duniani?

Kama miaka minne iliyopita alishindwa kuwaongezea maslahi yenu, sahau hilo kwa sasa. Dunia inapigana vita ya kiuchumi, hakuna nchi itaongeza maslahi ya watu wake, sana sana muombe mifuko ya jamii iweke recovery package kwa ajili ya wafanyakazi kipindi hiki kigumu, walau 20% ya savings zenu.
Hata corona isingekuwapo asingeongeza, muhimu vitu kwanza ndio vyenye kiki
 
Nahodha bora hawezi kukizamisha chombo chake majini! Ajitokeze hadharani aje aongoze mapambano badala ya kujificha kijijini na kukiacha chombo kijiendee chenyewe. Hii Corona inasafiri kama umeme! Itamtafuta tu kokote kule alikokimbilia.

Labda atubu hadharani dhambi zake zote alizotutendea kwa miaka yote hii 5! Huenda atasamehewa.
Jiwe kwenye shida ni kokoto tu,ujiwe upo kwenye kumshughulikia mbowe
 
Yaani wakati wafanyakazi sekta binafsi wananyimwa mishahara Na kupewa likizo zisizo Na malipo serikali IPO tu....
 
Wewe kama ni jobless shauri yako,wafanyakazi Wa sekta zote za umma wameongezwa mishahara kimya kimya ,ndio maana huwezi sikia migomo wa kelele zozote ,na wanapokea kwa wakati ,tofauti na enzi za Jakaya Kikwete

Wanaolalamikaga mitandaoni ni masela tu kama wewe
Kwenye hizo salamu sijaona sehemu yoyote aliyozungumzia masrahi ya wafanyakazi yaan najaribu kuvuta picha ya mabango ambayo angebebewa Leo daaaah!!! Alipo anamshukuru saana Mungu maana sijui angesema nini Leo nadhani angepata wakati mgumu kuandaa speech ya Leo maana alikuwa hana akiba ya neno hata moja yooooote alikuwa ameshayatumia/kuyaongea eg: "kabla sijatoka madarakani nitakuwa nimeshaongeza mshahara" alisikika abiria mmoja akisema

#tumechoka kudanganywa
#tunataka haki zetu

*Pamoja na kuwepo Corona lakini tukumbuke maisha yanaendelea

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilifikiri atakuja na kauli juu ya wafanyakazi wa sekta binafsi wanaochishwa kazi kiholela na kuzuiwa malipo yao kipindi hiki,pia mpango madhubuti wa kumpa relief mfanyakazi katika kipindi hiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ameshawambia waajiri wasiwanyanyase wafanyakazi kwa kisingizio cha korona..
 
Back
Top Bottom