Salaam hizi zinatumwa kutoka wapi?
Sent using
Jamii Forums mobile app
SALAMA HIZI ZAWEZA ATHIRIWA NA UTAMBULISHO KWA MAANA YA IDENTITY.
Utambulisho wa sehemu au identity hubadilika kutokana na mazingira, muda, hali, umri, rika, hadhi, mtazamo, kundo la watu, na kadha wa kadha.
Ipo hivi ukiwa nyumbani kwako utambulisho wako hubadirika kutokana na sababu nilizo ainisha hapo juu. Ukiwa nyumbani waweza tambulika kama "Jirani", "Baba", "Mume", "Mke", "Mama", "Mkwe", "Mtoto", "Kaka", "Dada" na kadha. inategemea upo katika kundi la namna gani.
Ila ukitoka na ukiwa watembea kwa miguu utambulishi wako utabadilika tena, hapa utatambulika kama "mwenda kwa miguu" au "mpita njia" au "mwananchi" au "raia" nk.
Ukipanda daladala au bodabaoda utambulisho wako pia utabadilika na kuwa "abiria". kwa bahati isio njema ukipata ajali na kunusurika basi utambulisho wako utabadirika pia na kuwa "manusura wa ajari" au "majeruhi" na ukienda lazwa hospitali basi utambulisho wako pia utabadirika na kuwa "mgonjwa". Ikitokea umeaga basi utambulisho wako utakuwa "marehemu".
Kwa hali hiyo hiyo ya tabia ya utambulisho, huenda basi huathiri eneo alilopo rais kwa wakati huo, na shughuli aifanyayo.
Kama ulivyo mwenge wa uhuru ile risala ya utii husamwa kwa kuelekezwa kwa Mh Rais so inamaana uonapo mwenge wa uhuru unaashiria uwepo wa rais.