Mei Mosi imekaribia, Rais Samia andaa neno/tendo la faraja kwa watumishi wako waaminifu

Fukua

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2022
Posts
546
Reaction score
479
Watumishi ambao ni daraja kati ya serikali na wananchi wanaisubiri hii siku kwa matumaini makubwa sana.

Kundi hili lilibanwa mbavu na raisi aliyekutangulia ingawa haikuwa kwa Nia mbaya Bali kufunzwa uzalendo kwamba Kuna wakati wa kuumia kwa ajili ya wengine.

Walivumilia na kukomaa japo haikuwa rahisi hata kidogo na matunda ya uvumilivu wao yalionekana kwani Kuna miundo mbinu mingi sana ilijengwa.

Uliposhika uskani uliongeza WiGo wa kutafuta pesa kwa ajili ya miradi mikubwa pia uliona inafaa kuwarudishia kile kidogo AAA kikubwa sana kilichobanwa. Jambo hili lilirudisha matumaini upya kwani ilifikia Hawa watumishi hasa wa ngazi za chini kuishi kama mashetani na kushindwa kutunza familia zao. Kwani waliachwa mbali sana na gharama za maisha.

Hivyo mama wengi wanategemea huu mwendelezo mwema, uwaongezee watumishi wako mishahara, kuwapandisha madaraja na kuboresha maslahi yao, ili waendelee kuwa daraja imara la kupitisha maendeleo kuyapeleka kwa wananchi.

Ahsante mama watumishi wana Imani na wewe.

Mungu akulinde na kukutunza
 
Mheshimiwa Rais Watumishi wana imani na wewe sema neno hiyo mei mosi watumishi wapone hasa kuhusu malimbikizo ya tangu 2016 na 2017 kwa kuagiza yalipwe within muda fulani kwani yamehakikiwa miaka kibao iliyopita ni utashi wa kulipa tu umekosekana.
 
Ukimtegemea MWANASIASA unaweza pata pressure buree kabisa.

Mwanasiasa ni mtu asiyeaminika kabisa tena aliyejaa UBINAFSI, japo Samia ana kitu cha tofauti kidogo.

SIRI KUBWA KATIKA MAFANIKIO YOYOTE YALE AU MAENDELEO NI KUWALIPA VIZURI WATUMISHI.
 
Watumishi ambao ni daraja kati ya serikali na wananchi wanaisubiri hii siku kwa matumaini makubwa sana.

Kundi hili lilibanwa mbavu na raisi aliyekutangulia ingawa haikuwa kwa Nia mbaya Bali kufunzwa uzalendo kwamba Kuna wakati wa kuumia kwa ajili ya wengine.

Walivumilia na kukomaa japo haikuwa rahisi hata kidogo na matunda ya uvumilivu wao yalionekana kwani Kuna miundo mbinu mingi sana ilijengwa.

Uliposhika uskani uliongeza WiGo wa kutafuta pesa kwa ajili ya miradi mikubwa pia uliona inafaa kuwarudishia kile kidogo AAA kikubwa sana kilichobanwa. Jambo hili lilirudisha matumaini upya kwani ilifikia Hawa watumishi hasa wa ngazi za chini kuishi kama mashetani na kushindwa kutunza familia zao. Kwani waliachwa mbali sana na gharama za maisha.

Hivyo mama wengi wanategemea huu mwendelezo mwema, uwaongezee watumishi wako mishahara, kuwapandisha madaraja na kuboresha maslahi yao,
Ili waendelee kuwa daraja imara la kupitisha maendeleo kuyapeleka kwa wananchi.

Ahsante mama watumishi wana Imani na wewe.

Mungu akulinde na kukutunza
Mimi ninachotaka tu amfute kazi Ridhiwani Kikwete na kumfunga kwa kulitia hasara taifa letu. Kingine atoe tamko la kukamata hawa mawaziri Mwigulu Nchemba, January Makamba, Nape Nnauye kwa ufisadi wao
 
Mheshimiwa Rais Watumishi wana imani na wewe sema neno hiyo mei mosi watumishi wapone hasa kuhusu malimbikizo ya tangu 2016 na 2017 kwa kuagiza yalipwe within muda fulani kwani yamehakikiwa miaka kibao iliyopita ni utashi wa kulipa tu umekosekana.
Leo watumishi mtalala kwa furaha sana. Mama ni msikivu amesikia na kutatua kero zenu kwa asilimia 95%
 
Back
Top Bottom