Mei Mosi Mwanza: Rais Samia ahutubia, aahidi kuongeza mishahara kuanzia mwakani, agusia mafao ya wastaafu

Mama Samia ; sekta binafsi miaka 8 hawajapandishiwa mshahara, hapa nadhani mama kateleza,sekta binafsi gani hiyo miaka 8 hawajapandishiwa mishahara
Kima cha chini sekta binafsi ni kiasi gani ??

Na mara ya mwisho kupandishwa ni lini??
 
Mpeni mama muda, ni muda mfupi mno kubalance mambo na kuanza kuongezea watu mishahara...Tayari nchi ilikuwa kwenye direction ya mtu mwingine na mtazamo wake, kwa miezi miwili ni ngumu kuitoa huko na kuiweka kwenye direction na mtazamo mwingine..
 
Nawasalimu kwajina la jamuhuri ya muungano ya Tanzania.
 
Serikali inapaswa kuweka kiwango kimoja cha mishahara kwa nchi nzima na kiwe kwa sekta zote binafsi na umma.

Hivyo kima cha chini kiwe ni kisheria ni hiyo inayopendekezwa ya 970k kwa mwezi.

Sasa hiyo ni nani katika Tanzania hii anaweza kukulipa iwe serikali au sekta binafsi?

Cha msingi ni kutafuta kiwango kipya kimoja kwa sekta zote na kiwe ndo sheria kwamba watumishi walipwe.
 
Basi mfufue huyo MWANAUME wako aje kuwatesa watu na kuwateka wengine kibao kama alivyowateka Azory, Ben Saa 8, Roma na kujaribu kumuua Tundu Lissu. Acha kunitafutia ban wewe mpuuzi!
 
Hali ya uchumi hairuhusu kupandishwa mshahara naona Mama kawaskiliza washauri wake wa masuala ya Kiuchumi kudos to Mama SSH
Hajaamua kufanya siasa. Hakika kwenye hili wale ambao tuna elimu ya uchumi japo kidogo tuliliona.

Hali ya uchumi worldwide imeathiriwa na COVID-19.
 
maza kacheza kama pele, lile shangwe zito limezimwa kama mshumaa
 
Serikali waache kujigamba tumepanda uchumi wakati hatuna corona lakini likija suala la mishahara ohhh uchumi hauko sawa na corona imeleta shida ila viongozi wa siasa tuliwasikia dunia nzima wanahangaika sisi tunadunda tu. tuache kujisifia kama tuko instangram hakuna cha uchumi wa kati wa nini yote number zilipikwa tu hakuna uhalisia.
 
Mpeni mama muda, ni muda mfupi mno kubalance mambo na kuanza kuongezea watu mishahara...Tayari nchi ilikuwa kwenye direction ya mtu mwingine na mtazamo wake, kwa miezi miwili ni ngumu kuitoa huko na kuiweka kwenye direction na mtazamo mwingine..
Ndio maana tunasema Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…