Mei Mosi Mwanza: Rais Samia ahutubia, aahidi kuongeza mishahara kuanzia mwakani, agusia mafao ya wastaafu

Tunasema kila siku humu kwamba mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu
Tanzania haina uchumi wa kulipa kima cha chini cha mishahara cha 970,000

Tufanye kazi kwa kujituma tukuze uchumi tuache kelele.

Pia tuache kupiga, wizi na ufisadi.
 
970k parefu sana mkuu, hao waajiri wa sekta binafsi wanaona hiyo 100k pia inawawekea kiwingu.
 
Kweli huyu mama leo kanigusa, kila mwaka nilikuwa naongeza deni wakati hata mategemeo ya kazi sina.
Pole sana mkuu.

Tumpeni mama muda na mambo yatakuwa mazuri. Karibu kwenye dua ya kumuombea mama itakayofanyika siku ya tarehe 8 May 2021 hapa michenzani Mall - Zanzibar
 
Mpeni mama muda, ni muda mfupi mno kubalance mambo na kuanza kuongezea watu mishahara...Tayari nchi ilikuwa kwenye direction ya mtu mwingine na mtazamo wake, kwa miezi miwili ni ngumu kuitoa huko na kuiweka kwenye direction na mtazamo mwingine..
Kweli kabisa mkuu! Hata hivyo Mama ana utu, Mungu amtie nguvu. Tutafika.

Ila mtanguliz wake.......... mmmmmh!
 
970k parefu sana mkuu, hao waajiri wa sekta binafsi wanaona hiyo 100k pia inawawekea kiwingu.
Naamini bado ipo dhamira ya kujenga Tanzania yenye uchumi bora.

Uchumi imara ni viwanda, miundombinu na teknolojia.

Bila haya mavitu Tanzania haiwezi kuja kumlipa mtumishi 970,000 kwa hali ya uchumi iliopo sasa.
 
Aisee
 
Uzi hautembei tena [emoji28][emoji28][emoji28]
 
Nani kama Mama Rais Samia ⁉️ Tayari amemaliza hotuba tama kama asali kwa wafanyakazi ❕ Wafanyakazi wenyewe wanasemaje sasa kuhusu kauli mbiu yao kwa mwaka huu ❓
 
Mkuu tupe neno LA hekima ilikuwaje akatundika daluga huko Serikalinijitoe,na badaye ulijishughulisha na nini ama ilikuwaje??
Nia ni kujifunza,maana wengine tukiwa huku ndio tunafikiria maisha ni huku tu.
Niliamua nikatoka nikaenda chuo nikakatiwa mshahara, sikujali, nilipomaliza chuo nikasoto kidogo mitaani nikaanza ujasiliamali, baadae nikaenda kusoma tena.sasa hivi namshukuru mungu hicho kidogo nachopata ni haki yangu na nakifanyia kazi.

Kwenye hiki kipindi mnachoikiita cha jpm ndo kipindi watu tumepata vikazi hata kama ni vidogo lakini tunapata chochote.

Ukitaka kuishi maisha yasio ya stress usitegemee mshahara.
 
Wale wanaolalamikia mishahara, ahadi ya mama inaponya sana. Mwakani siyo mbali kabisaaa! Angalau sasa wanaweza kuishi kwa matumaini sana. Na ninaamini Rais hatoweza kubatilisha ahadi ya namna hii mana hajasema "mwakani tutaangalia!" Bali "mwakani mwezi kama huu nitawaongezea mishahara!"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…