Mei Mosi Mwanza: Rais Samia ahutubia, aahidi kuongeza mishahara kuanzia mwakani, agusia mafao ya wastaafu

Mei Mosi Mwanza: Rais Samia ahutubia, aahidi kuongeza mishahara kuanzia mwakani, agusia mafao ya wastaafu

Tunasema kila siku humu kwamba mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu
Tanzania haina uchumi wa kulipa kima cha chini cha mishahara cha 970,000

Tufanye kazi kwa kujituma tukuze uchumi tuache kelele.

Pia tuache kupiga, wizi na ufisadi.
 
Serikali inapaswa kuweka kiwango kimoja cha mishahara kwa nchi nzima na kiwe kwa sekta zote binafsi na umma.

Hivyo kima cha chini kiwe ni kisheria ni hiyo inayopendekezwa ya 970k kwa mwezi.

Sasa hiyo ni nani katika Tanzania hii anaweza kukulipa iwe serikali au sekta binafsi?

Cha msingi ni kutafuta kiwango kipya kimoja kwa sekta zote na kiwe ndo sheria kwamba watumishi walipwe.
970k parefu sana mkuu, hao waajiri wa sekta binafsi wanaona hiyo 100k pia inawawekea kiwingu.
 
Mpeni mama muda, ni muda mfupi mno kubalance mambo na kuanza kuongezea watu mishahara...Tayari nchi ilikuwa kwenye direction ya mtu mwingine na mtazamo wake, kwa miezi miwili ni ngumu kuitoa huko na kuiweka kwenye direction na mtazamo mwingine..
Kweli kabisa mkuu! Hata hivyo Mama ana utu, Mungu amtie nguvu. Tutafika.

Ila mtanguliz wake.......... mmmmmh!
 
970k parefu sana mkuu, hao waajiri wa sekta binafsi wanaona hiyo 100k pia inawawekea kiwingu.
Naamini bado ipo dhamira ya kujenga Tanzania yenye uchumi bora.

Uchumi imara ni viwanda, miundombinu na teknolojia.

Bila haya mavitu Tanzania haiwezi kuja kumlipa mtumishi 970,000 kwa hali ya uchumi iliopo sasa.
 
Mama hatataja kuongeza mshahara Ila atatoa kauli ya kuwa wahusika wangalie namna ya kuongeza maslahi kwa watumishi kwa kuzingatia muda ambao hawajafanyiwa hivyo. Ataomba busara kwa watumishi wampe muda kupitia idara husika wakamilishe mchakato japo ni ndani ya mwaka huu huu
Aisee
 
May Day , May Day, SOS we need help, we need increment
IMG-20210501-WA0019.jpg
 
Kutoka jijini Mwanza tunawaletea taarifa za moja kwa moja, maadhimisho ya sherehe ya siku ya wafanyakazi duniani,ambayo kitaifa yanafanyika hapa.

Mgeni rasmi anatarajiwa kua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mama Samia Suluhu Hassan, ambapo atapokea maandamano ya wafanyakazi mbalimbali Tanzania.View attachment 1769649

Hali ya hewa ni tulivu kabisa,uwanja umepambwa vyema,barabara za jiji zimesafishwa safi huku zikichagizwa na mabango yenye ujumbe wa hapa na pale.

Wananchi wameanza kumiminika viwanjani hapa.

Karibuni.....
============
Updates.
Tayari uwanjabwa ccm kirumba umeanza kufurika huku ukipendezeshwa na sare mbalimbali za tishirts na kofia za vyama vya wafanyakazi wa sekta binafsi,serikali kuu,mashirika ya umma,serikal za mitaa,na chama cha walimu,nyuso za wafanyakazi zinaonyesha tabasamu lililojaa matumaini tofauti na mei mosi za miaka 5 iliyopita.

Viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya wafanyakazi wameanza kuwasili uwanjani.
Namuona Makamu wa Rais,Dr.Mpango,Waziri Mkuu Majaliwa,Katibu Mkuu Kiongozi,Spika wa bunge na makamu wake.
View attachment 1769738
===========
Updates
Tayari msafara wa Rais Mama Samia umewasili uwanja wa CCM Kirumba tayari kwa shughuli za Mei Mosi kuanza rasmi,shangwe na nderemo zinashamiri uwanjani hapa wananchi wakimshangilia Rais wetu.View attachment 1769780
======
Maandamano yanaanza baada ya Rais Samia kuwasili jukwaani,takribani vyama 17 vya wafanyakazi vitashiriki maandamano haya.View attachment 1769848
=========
Updates


1619866857440.png
Nani kama Mama Rais Samia ⁉️ Tayari amemaliza hotuba tama kama asali kwa wafanyakazi ❕ Wafanyakazi wenyewe wanasemaje sasa kuhusu kauli mbiu yao kwa mwaka huu ❓
 
Mkuu tupe neno LA hekima ilikuwaje akatundika daluga huko Serikalinijitoe,na badaye ulijishughulisha na nini ama ilikuwaje??
Nia ni kujifunza,maana wengine tukiwa huku ndio tunafikiria maisha ni huku tu.
Niliamua nikatoka nikaenda chuo nikakatiwa mshahara, sikujali, nilipomaliza chuo nikasoto kidogo mitaani nikaanza ujasiliamali, baadae nikaenda kusoma tena.sasa hivi namshukuru mungu hicho kidogo nachopata ni haki yangu na nakifanyia kazi.

Kwenye hiki kipindi mnachoikiita cha jpm ndo kipindi watu tumepata vikazi hata kama ni vidogo lakini tunapata chochote.

Ukitaka kuishi maisha yasio ya stress usitegemee mshahara.
 
Wale wanaolalamikia mishahara, ahadi ya mama inaponya sana. Mwakani siyo mbali kabisaaa! Angalau sasa wanaweza kuishi kwa matumaini sana. Na ninaamini Rais hatoweza kubatilisha ahadi ya namna hii mana hajasema "mwakani tutaangalia!" Bali "mwakani mwezi kama huu nitawaongezea mishahara!"
 
Back
Top Bottom