Mei Mosi ya 2023 imepooza! Shida nini?

Hii katuni inaweza kuwa na Uhusiano na Mei Mosi ya mwaka 2023?
 

Attachments

  • EFCAF7BA-8A76-46C5-86E5-C4606B95546F.jpeg
    78.8 KB · Views: 1
Hatahivyo majogoo haya, mihogo inayochemka mingine chelema, Chai haina sukari, Bodaboda bado anafukuza upepo simu haisikiki vizuri, waifu kanuna....hela ya kalamu huna ujiandikie hata kaujumbe kwenye karatasi inayosema "Bei Zimefumuka" au Mfumuko wa bei
"Tozo Karahaa" "Umeme Kalasi Nyumbani na Uwanjani, Awajibikwe"(hiyo makusudi)
Tutajua baadae.....

Imepooza lakini
 
Habari za Asubuhi wapendwa!

Binafsi nimeshangazwa na sikukuu ya wafanyakazi (Mei Mosi) ya mwaka 2023 kupoa, hakuna ata matangazo wala promo lolote! Kama vile hamna kitu kabisa!

Wafanyakazi tatizo nini?
Hata Mimi na shangaa hakuna hata amusha amusha au slogani, ya Nini wafanyakazi wanataka mwakahuu Hapo ndo ninapohitimisha kuwa vyama vya wafanyakazi vinaendeshwa na serikali.
 
Mimi naifatilia mei mosi ya majirani zetu Kenya live from uhuru garden.
 
Wafanyakazi wamechoshwa na ahadi hewa, huo ndio ukweli! Maan hawategemei kipya.
 
Umeiandika kiutani lakini inachoma sana moyoni.
 
Pole sana mwalimu, inahuzunishaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…