Meja Kunta unatisha una-deserve kupewa sifa

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Najua kuna baadhi ya watu ukitoa sifa kwa mtu hawapendi Mara utasikia umekuja kujipigia promo humu lakini tuwe wakweli this man called Meja kunta ameleta mapinduzi kiasi kikubwa kwenye singeli. Meja kunta ana voice unique sana na yenye mvuto tofauti na wasanii wengi wa singeli binafsi nilikuwa si mpenzi wa singeli ila tangu huyu mwamba aje nimekuwa mshabiki wake lakini pia kwa singeli kiujumla.

Kipaji alichonacho Meja kunta kawazidi wasanii wengi wa Bongo Fleva ana sauti fulani hata kama wimbo wa kawaida anaufanya uwe mkali. Kwa kazi nzuri anazofanya huyu mwamba anastahili pongezi kubwa.
 
Naukubali sana wimbo wake wa Mamu
 
ooonhooo onhoooo..
anhaaaa anhaaaaaa..
oooooooooooooooooh..
aaaaaaaaaaaaaaaaaaah..

hajui kuimba, analia na kupiga kelele kwenye nyimbo zake....

niliipenda singeli kupitia wimbo wa 'Rafiki wa kweli' ,nikaipotezea baadae, ikaanza ku kick kwa nyimbo za hainaga ushemeji, hujaulamba, etc...

hakuna msanii aliyebebwa na hajui kuimba kama huyo meja kunta, ..

kwasasa wimbo naosikiliza sana wa singeli ni 'GETO LA BIBI' wa Sholo mwamba... japo umetoka mwaka jana, mimi n mchaguzi sana wa nyimbo za kusikiliza ,ila nasema meja kunta hajui kaka, anapiga tu kelele..

na inawezekana alijua hajui ndiyo maana akajizushia kifo...

huwezi muweka kwenye kundi moja na kina MSAGA SUMU(LEGEND), DULA MAKABILA, SHOLO MWAMBA, SKIDE, au yule alomshirikisha MARIOO kwenye wimbo wa NAKUJA....

Kama kakutuma kamwambie feedback ni HAJUI, aendelee kutegemea promo ambayo ni mbaya na itamtesa baadae kama inavyowatesa wasanii walio itegemea Clouds fm enzi za Ruge kwa sasa wanalala njaa.
 
Hayo ni maoni yako sasa Meja kunta na sholo mwamba yupi anapiga makelele?
 
Huyu ndo aligair Kufa eeh kama skosey
 
Umeisikiliza ile aliyoshirikishwa na mtoto wa gadna...
 
Mzee wa
bwax bongo hii sijaona kwetu mbeya nyimbo zake walikuwa wanapiga Hadi kwenye makanisa hasa ile nyimbo inayoitwa kademu gangu kalokole
Kanisani loh!😲😲
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…