Meja Kunta unatisha una-deserve kupewa sifa

Meja Kunta unatisha una-deserve kupewa sifa

Msaga Sumu ndo msanii ambaye anakaaa kimya ila akitoka na ngoma anafunika waimba singeli wote
ooonhooo onhoooo..
anhaaaa anhaaaaaa..
oooooooooooooooooh..
aaaaaaaaaaaaaaaaaaah..

hajui kuimba, analia na kupiga kelele kwenye nyimbo zake....

niliipenda singeli kupitia wimbo wa 'Rafiki wa kweli' ,nikaipotezea baadae, ikaanza ku kick kwa nyimbo za hainaga ushemeji, hujaulamba, etc...

hakuna msanii aliyebebwa na hajui kuimba kama huyo meja kunta, ..

kwasasa wimbo naosikiliza sana wa singeli ni 'GETO LA BIBI' wa Sholo mwamba... japo umetoka mwaka jana, mimi n mchaguzi sana wa nyimbo za kusikiliza ,ila nasema meja kunta hajui kaka, anapiga tu kelele..

na inawezekana alijua hajui ndiyo maana akajizushia kifo...

huwezi muweka kwenye kundi moja na kina MSAGA SUMU(LEGEND), DULA MAKABILA, SHOLO MWAMBA, SKIDE, au yule alomshirikisha MARIOO kwenye wimbo wa NAKUJA....

Kama kakutuma kamwambie feedback ni HAJUI, aendelee kutegemea promo ambayo ni mbaya na itamtesa baadae kama inavyowatesa wasanii walio itegemea Clouds fm enzi za Ruge kwa sasa wanalala njaa.
 
Anajua ila kuna melody kazipiga kwenye mamu karbia kila wimbo wake utazikuta ,yaan anazunguka pale pale tu , mfikishie salamu kua anasauti Kali ila ubunifu zaid unahitajika kina balaa mc washaanza vurugu mjini
 
Anajua ila kuna melody kazipiga kwenye mamu karbia kila wimbo wake utazikuta ,yaan anazunguka pale pale tu , mfikishie salamu kua anasauti Kali ila ubunifu zaid unahitajika kina balaa mc washaanza vurugu mjini
Hiyo melody ndio silaha yake inayomtofautisha Kati yake na Wasanii wengine kwanini asiitumie na sawa na producers wanakuwa na touch zao kila Wimbo lazima ziwepo
 
Ndio aloimba namruhusu mke akadange
Hiyo nyimbo kali jamani
 
Mamu,Shori,Chura superstar,Wanga,,Muulize Swizz beat anamjua vizuri uyu dogorasi Kunta
 
Najua kuna baadhi ya watu ukitoa sifa kwa mtu hawapendi Mara utasikia umekuja kujipigia promo humu lakini tuwe wakweli this man called Meja kunta ameleta mapinduzi kiasi kikubwa kwenye singeli. Meja kunta ana voice unique sana na yenye mvuto tofauti na wasanii wengi wa singeli binafsi nilikuwa si mpenzi wa singeli ila tangu huyu mwamba aje nimekuwa mshabiki wake lakini pia kwa singeli kiujumla.

Kipaji alichonacho Meja kunta kawazidi wasanii wengi wa Bongo Fleva ana sauti fulani hata kama wimbo wa kawaida anaufanya uwe mkali. Kwa kazi nzuri anazofanya huyu mwamba anastahili pongezi kubwa.
Mkuu unamjua Balaa Mc?
 
Jamaaa anajua sana .

Kama huu wimbo wa demu wangu ni hatari na nusu kuanzia audio mpaka video
 
Back
Top Bottom