Melania Trump ataka Tshs Milioni 675 ili kufanya mahojiano na CNN. CNN yajibu mapigo!

Melania Trump ataka Tshs Milioni 675 ili kufanya mahojiano na CNN. CNN yajibu mapigo!

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Shirika la habari la Marekani, CNN, limeripoti kuwa wakati waandishi wake wakiwa wanajaribu kupata mahojiano na mke wa rais wa zamani wa Marekani, Melania Trump, team ya Melania Trump ambao wanahusika na uchapishaji wa kitabu chake kipya ilijibu ilitaka kiasi cha dola 250,000, zaidi ya shilingi milioni 675 za Kitanzania kufanikisha mahojiano hayo.

Kupitia barua pepe iliyotumwa na CNN kwa kampuni ya Skyhorse Publishing ilijumuisha hati yenye kichwa "Mkataba wa Usiri na Kutofichua," ambayo iliweka masharti magumu ya kufanikisha mahojiano hayo.

Soma pia: Eti gauni alilovaa leo Melenia Trump akienda kupiga kura ni shilingi millioni 15

Hata hivyo, CNN ilikataa kulipa kiasi hicho cha fedha ili kupata mahojiano na Melania Trump.

Melania.png

Baada ya siku chache, mwanahabari mwingine wa CNN alipoiuliza Skyhorse Publishing kuhusu gharama hiyo kubwa ya mahojiano, mchapishaji huyo alieleza kuwa ombi hilo la malipo kwenda kwa CNN lilitumwa kimakosa.

Malipo kwa watu maarufu kwa ajili ya mahojiano, hasa kwa wake wa wagombea wa kisiasa, ni jambo lisilo kubalika katika vyombo vingi vya habari nchi Marekani

Source: CNN
 
Back
Top Bottom