Biblia inamtambua Maria kama mama yake Yesu, Tena ni maneno ya Malaika wa Bwana.
Kwa hiyo sisi tunamsikiliza malaika wa Bwana zaidi siyo wewe unayesema Maria siyo mama yake Yesu ila "ni kibebo cha mimba(surrogate) tu
Mathayo: 2: 19-21 Inasema
19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, "Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa." 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israel