Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Mkuu hata sisi binadamu tunamuita Mungu ni Baba na Yesu ni kaka yetu ila Je hatuna baba wa kimwili??
Yohana 1:12
12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
Wakolosai 1:15
15 naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.
Anaitwa mwanaye sababu ana Roho wa Mungu ndani yake na sisi pia tunaitwa watoto wa Mungu sababu tuna Roho wake ndani yetu lakini sio Baba kimwili.
So Still Yesu hana Baba wala Mama coz alikuwepo kabla hata ya uumbaji ila huyo Maria alitumika kma njia ya kumleta duniani ila sio kwamba ndio alimzaa Yesu tokea dunia haijaumbwa.
So bado Yesu hana Baba wala Mama na anathibitisha hapa
Mathayo 12
46 Alipokuwa katika kusema na makutano, tazama, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wataka kusema naye.
47 Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe.
48 Akajibu, akamwambia yule aliyempasha habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani?
49 Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu!
50 Kwa maana ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.
Bwana Zitto Junior hebu fafanua hili la Yesu kuitwa Mzaliwa wa kwanza wa viumbe wote, hii maana yake ni nini?
(Wakolosai 1:15 )
Pili unasema Yesu ana roho wa Mungu ndani yake na unasema pia na sisi pia tuna roho wa Mungu ndani yetu, Je utofauti wa Roho wa Mungu aliyemo ndani ya Yesu na yule aliyemo ndani yetu ni nini?