Melchizedek na utata unaomzunguka

Melchizedek na utata unaomzunguka

Kuna andiko linasema Mungu ni mfalme wa amani

Andiko jingine linasema Melkizedeki ni mfalme wa Salem ( Amani)

Wenye kupenda kuungaunga maandiko wanaequate Amani adjective na Amani( noun yaani jina la mji), Then wanaconclude kuwa maadam kwenye andiko moja Mungu anaitwa Mfalme wa amani, na kwa kuwa kwenye andiko jingine Melkizedeki ametajwa kuwa alikuwa mfalme wa Salem basi eti Hiyo ni clue kuwa Melkizedeki ni Mungu. Na kwa kuwa watu hao huwa wanaamini kuwa Mungu ni Yesu kwa hiyo Melkizedeki ndiye huyohuyo Yesu.

Huko ni kuungaunga kwenye maandiko

Salem ni jina la Zamani la Yerusalem
 
Hizi ngonjera ndio waga nazikata, kwaiyo wakiandika "Yesu akaenda Galilaya" ukitumia akili zisizo za kimamalia kama usemavyo ndio itasomeka Yesu akaenda msumbiji au....!!!? Tusichoshane[emoji124][emoji124][emoji124]
Utaambiwa galilaya ni mji wa pili kwa ukubwa huko mbinguni tukianza na jerusalemu
 
Kuna andiko linasema Mungu ni mfalme wa amani

Andiko jingine linasema Melkizedeki ni mfalme wa Salem ( Amani)

Wenye kupenda kuungaunga maandiko wanaequate Amani adjective na Amani( noun yaani jina la mji), Then wanaconclude kuwa maadam kwenye andiko moja Mungu anaitwa Mfalme wa amani, na kwa kuwa kwenye andiko jingine Melkizedeki ametajwa kuwa alikuwa mfalme wa Salem basi eti Hiyo ni clue kuwa Melkizedeki ni Mungu. Na kwa kuwa watu hao huwa wanaamini kuwa Mungu ni Yesu kwa hiyo Melkizedeki ndiye huyohuyo Yesu.

Huko ni kuungaunga kwenye maandiko

Salem ni jina la Zamani la Yerusalem
Unapoongea kuhusu aya za Biblia ni vema kuleta vifungu, sio utashi. Mambo ya kuna andiko hayana mashiko, ni habari za vijiwe vya kahawa.

Hebu fikiri, Melkizedeki alikuwa kuhani wa Mungu aliye juu sana , wakati ambapo Mungu huyo huyo hakuwa ameanza mpango wa ukombozi wa mwanadamu. Ibrahim ndiye aliyeanzisha mpango huo, baada ya Mungu Mwenyezi kuamua kumtumia. Kwa maana nyingine Mungu alikuwa na taifa linalomwabudu kabla ya kuitwa kwa Ibrahim kuanzisha uzao wa wana wa Israeli. Taifa hilo ni la Salem ambapo mfalme wake alikuwa Melkizedeki.

Biblia ni mwunganiko, kwa wenye kuisoma kwa uhalisia wake. Ila kwa kukariri mstari mmoja mmoja ndipo tunapata hoja kama hii yako. Ni ajabu kwamba hata ufafanuzi wa Biblia yenyewe unaupunga na kuuita kuungaunga maandiko. Kama unapinga Waraka kwa Waebrania kwa hoja zako za kufikirika sina jinsi ya kukusaidia. Shikilia hicho unachokiamini.
 
Mh...Tuzidi kusali
Kusoma neno la Mungu hadi uelewe inahitaji uombe kwanza roho mtakatifu afungue fahamu zako

Hata wale wanafunzi wa Yesu kuna mda walikua hamwelew wakamwomba awatafsirie
 
Hii ni mojawapo ya masomo ambayo nimeyapitia kwa undani kidogo. Sijui kama kuna nafasi ya kutosha. Lakini kwa ufupi niseme tu Mwandishi wa Waebrania, wa Zaburi na yule wa Mwanzo wote wanamzungumzia mtu yule yule; Yesu Kristu. Kumbuka Waebrania ina mstari mmoja muhimu sana Waeb. 13.8 ambayo inasema "Yesu Kristu ni yule yule, Jana, na leo, na hata milele". Na kama unakumbuka katika unabii wa Isaya kuhusu kuzaliwa kwa Yesu tunaambiwa kati ya majina yake mengi mojawapo ataitwa "Mfalme wa Amani"... Mfalme wa Amani ni Mfalme wa Salemu (Salemu ni "amani").

Hii ndio sababu Ibrahim alipokutana na Melkizedek alimpa fungu la kumi (kumbuka hii ilikuwa kabla ya zaka kuingizwa katika sheria za wayahudi). Ukitaka kuelewa hili rejea maneno ya Yesu ambayo anawaambia Wayahudi kuwa "Ibrahim baba yenu aliitamani kuiona siku yangu, aliiona na akafurahi (Yoh 8:56). Na utaona kuwa Yesu hamuiti Ibrahimu "baba yetu" bali "baba yenu"... Lakini pia alitoa dai moja sehemu nyingine (mistari miwili tu chini) ambalo nusura wayahudi wampige. Alisema katika mstari mwingine maarufu "Kweli kweli nawaambia" Yesu akasema, "kabla Ibrahim hajazaliwa mimi Niko" (Yoh 8:58).

Basi hapo kwa ufupi tu; ni sehemu ya tafiti yangu moja ndefu sana; labda siku moja ikimpendeza Mungu nitawashirikisha.
Wewe mtu umesoma theology, unajua hadi unakera, hapo mtu mwenye akili achomoki.
 
Kuna kauli moja ina maana ikiitafakari.Nitaweka maneno haya kwa ajili ya tafakari zaidi
1Samweli 8:4~7

"4 Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea samweli huko Rama 5.wakamwambia, Angalia,wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote 6.lakini neno hilo likawa baya machoni pa samweli, waliposema,,tupe mfalme atuamue.Naye samweli akamwomba Bwana
7.Bwana akamwambia Samweli, ISIKILIZE SAUTI YA WATU HAWA KATIKA KILA NENO WATAKALOKUAMBIA; KWA MAANA HAWAKUKUKATAA WEWE, BALI WAMENIKATAA MIMI ILI NISIWE MFALME JUU YAO.

Cha kuzingatia hapa ni kwamba kulikuwa na uhusiano gani kati ya kuhani mkuu na Mungu katika kuongoza nchi?

Je! Mungu alikuwa mfalme kivup?
Nafasi ya kuhani mkuu ilikuwa na mahusiano gani na Mungu?
 
Nikirudi kwenye maada utaona katika Hekalu lililokuwa Jerusalem lilikuwa na partition tatu.Partition ya kwanza hema la kukutania,,partition ya pili hema ya kati sehemu ya sadaka zote na partition ya tatu patakatifu pa patakatifu,,,,,,,,,,,,Hii hema ya tatu aliingia mtu mmoja tu Kuhani mkuu tena akiwa amefungwa kamba mguuni ili incase kaingia na doa la dhambi akafa aweze kuvutwa nje mpaka apatikane tena kuhani mkuu mlawi aweze kuingia tena humo.

Hii itakuonyesha kwamba kuhani mkuu akiwa kama yeye alikuwa na nafasi kubwa sana ambayo ilimfanya wa kipekee maana ndie alieweza kwenda mbele za Mungu kwa kupewa dira ya nchi na kutubia dhambi ya nchi nzima.

Sasa huyo melickzedech kama kuhani mkuu katika ulimwengu halisi yanakofanyika Mambo halisi hafanyi tena upatanisho kwa kuashiria ila kwa uhalisia wake,,kitendo cha Ibrahim kumtolea fungu la kumi na kumsujudia kimeonyesha kwamba hakuwa binadamu na ile sadaka kuhusianishwa na kabila la lawi ambalo lilikuwa makuhani tu kuliashiria mwanzo wa ibada ya ishara yenye kufanana na ibada halisi ilio mahali flani..Na kilichofanyika na Israel ya zamani katika mwili kilikuwa ni ishara ila yenye mafungamano na mambo halisi katika ulimwengu mwingine
1. Melkizedeki Alikuwa ni kuhani wa Mungu alie juu au kuhani mkuu ?
2. Ibrahim alibarikiwa na Melkizedeki au alimsujudia ?
3. hapa duniani Yesu alikuwa na mama lakini Melkizedeki hakuwa na mama, vip wawe sawa hawa watu wawili ?
 
Kuna kauli moja ina maana ikiitafakari.Nitaweka maneno haya kwa ajili ya tafakari zaidi
1Samweli 8:4~7

"4 Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea samweli huko Rama 5.wakamwambia, Angalia,wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote 6.lakini neno hilo likawa baya machoni pa samweli, waliposema,,tupe mfalme atuamue.Naye samweli akamwomba Bwana
7.Bwana akamwambia Samweli, ISIKILIZE SAUTI YA WATU HAWA KATIKA KILA NENO WATAKALOKUAMBIA; KWA MAANA HAWAKUKUKATAA WEWE, BALI WAMENIKATAA MIMI ILI NISIWE MFALME JUU YAO.

Cha kuzingatia hapa ni kwamba kulikuwa na uhusiano gani kati ya kuhani mkuu na Mungu katika kuongoza nchi?

Je! Mungu alikuwa mfalme kivup?
Nafasi ya kuhani mkuu ilikuwa na mahusiano gani na Mungu?
1. KUHANI ni mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu , Melkizedeki alikuwa ni kuhani tu wala hakuwa kuhani mkuu ili kwanza ulijue
2. Mungu ni mfalme , Mungu ni mwenye wivu , Mungu ni mtu wa vita ,sioni ajabu Mungu kufanana baadhi ya sifa na watu wake mwenyewe ata mimi nina wivu kama Mungu , vile vile watu wa vita wamejaa duniani , hivyo hoja ya sifa hii ya mfalme haina mashiko, kwasababu sio jambo geni baadhi ya sifa kufanana kati ya Mungu na binadamu
 
Unapoongea kuhusu aya za Biblia ni vema kuleta vifungu, sio utashi. Mambo ya kuna andiko hayana mashiko, ni habari za vijiwe vya kahawa.

Hebu fikiri, Melkizedeki alikuwa kuhani wa Mungu aliye juu sana , wakati ambapo Mungu huyo huyo hakuwa ameanza mpango wa ukombozi wa mwanadamu. Ibrahim ndiye aliyeanzisha mpango huo, baada ya Mungu Mwenyezi kuamua kumtumia. Kwa maana nyingine Mungu alikuwa na taifa linalomwabudu kabla ya kuitwa kwa Ibrahim kuanzisha uzao wa wana wa Israeli. Taifa hilo ni la Salem ambapo mfalme wake alikuwa Melkizedeki.

Biblia ni mwunganiko, kwa wenye kuisoma kwa uhalisia wake. Ila kwa kukariri mstari mmoja mmoja ndipo tunapata hoja kama hii yako. Ni ajabu kwamba hata ufafanuzi wa Biblia yenyewe unaupunga na kuuita kuungaunga maandiko. Kama unapinga Waraka kwa Waebrania kwa hoja zako za kufikirika sina jinsi ya kukusaidia. Shikilia hicho unachokiamini.

Tatizo siyo waraka wa Waebrania, Tatizo ni uelewa wa waraka huo
Nyinyi mnautafsiri out of context kwa kuungaunga maana.

Ngoja Niquote Maandiko

SOURCE: https://www.biblegateway.com/passage/?search=Waebrania+7&version=SNT

Yesu Na Melkizedeki (Waebrania 7:11-17)
11 Kama ukamilifu ungaliweza kupatikana kwa njia ya ukuhani wa Walawi, kwa maana watu walipewa sheria kupitia kwao, ilikuwapo haja gani tena ya kuwepo kuhani mwingine, yaani kuhani kama Mel kizedeki, ambaye si kama Aroni? 12 Kwa maana yanapotokea maba diliko kwenye ukuhani, ni lazima pawepo na mabadiliko katika she ria. 13 Maana Bwana wetu ambaye ndiye anayesemwa katika mambo haya, alikuwa ni wa kabila lingine, na hakuna mtu katika kabila lake aliyewahi kuhudumu katika madhabahu. 14 Inafahamika wazi kuwa Bwana wetu alitoka katika kabila la Yuda, na Mose hakuwahi kusema lo lote juu ya makuhani kutoka katika kabila hilo. 15 Na hili tunalosema linakuwa wazi zaidi anapotokea kuhani mwingine kama Melkizedeki; 16 ambaye ukuhani wake hautokani na kanuni za ukoo wake, bali hutokana na uwezo wa maisha yasiyoharibika. 17 Kwa maana ameshuhudiwa hivi: “Wewe ni kuhani milele, kama wa Melkizedeki.”

Ni dhahiri:
Kwa mujibu wa andiko hilo katika msitari wa mwisho nilioupigia msitari unaosema "WEWE NI KUHANI MILELE KAMA MELKIZEDEKI" inaonysha kuwa YESU ni YESU na MELKIZEDEKI ni MELKIZEDEKI ila wote wana Ukuhani wa Milele!.

Neno "Kama" limetumika kwenye hilo andika KULINGANISHA watu wawili, Nikisema Mtu X kama Mtu Y kwenye ishu Z maana yake siyo kwamba X ndiye Y bali hawa ni watu tofauti lakini wana role Z ambayo ni moja

KITU KIKISHAITWA "KAMA" MAANA YAKE KINAFANANISHWA (compared to) , KINAKUWA SIYO CHENYEWE HALISI!

Ni suala la lugha tu, Ukitaka kutumia logic yako kuungaunga visivyoungika basi bible unaweza kuitafsiri vyovyote unavyopenda na ikaleta justification zozote
 
Hapa ndipo penye shida watu wakisema Magufuli kama Nyerere wao sijui wanaelewaje!!! kuna tatizo kwenye matumizi ya lugha hii , lakini wafahamu kuwa Magufuli sio Nyerere
 
1. Melkizedeki Alikuwa ni kuhani wa Mungu alie juu au kuhani mkuu ?

Melkizedeki hakuwa "Kuhani Mkuu" bali "Kuhani wa Mungu aliyejuu sana". Kumbuka wakati huo Mungu aliye juu sana hakuwa amefunuliwa kwa Musa na wala Ukuhani haukuwepo. Lakini tunadokezwa tu kuwa huyu Melkizedeki tayari alikuwa anamtolea sadaka El Elyon (Mwenye Enzi)

2. Ibrahim alibarikiwa na Melkizedeki au alimsujudia ?
Swali zuri sana; itabidi turudi kwenye text yenyewe. Lakini kiufupi ni kuwa Ibrahim alimpa heshima kubwa Melkizedeki na ndio pointi ya baadaye kwenye Waebrania. Kuwa kama Ibrahim alitoa fungu la kumi kwa Melkizedeki ina maana kiwadhifa au hadhi Melkizedeki alikuwa juu yake.

3. hapa duniani Yesu alikuwa na mama lakini Melkizedeki hakuwa na mama, vip wawe sawa hawa watu wawili ?

Hili ni swali zuri. Na hapa ndio wengi wanachanganyikiwa. Je, Yesu alikuwepo kabla ya Bikira Maria; au alianza kuwepo baada ya kuzaliwa? Dokezo kidogo ni kuwa katika ile inayojulikana kama "Sala ya Kikuhani" ya Yesu kwenye Yohana 17 tunakutana na ombi hili kwa babake "Na sasa Baba, nitukuze mbele zako kwa ule utukufu niliokuwa nao kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu" (Yoh. 17:5). Na mistari kadhaa chini anasisitiza hili (Yoh. 17:24). Ukisoma mistari hiyo lazima ujiulize? Yesu alikuwepo kabla ya misingi ya ulimwengu? Na kama alikuwepo kuzaliwa kwake na Bikira Maria basi kuna maana gani?
 
Duu kama mwandishi wa kitabu cha waebrania hajulikani basi atakua ni babu wa kizazi cha hawa jamaa wasiojulikana ambao walimchabanga risasi ndugu Tindu Lissu.
 
Missile of the Nation, nitakusaidia tu hapa kidogo. Unafanya kosa moja kubwa. Ni kuwa unadhania waraka wa Waebrania uliandikwa kwa Kiswahili. Niseme tu kuwa ukisoma huo mstari kwa mfano kwenye Kiingereza hausemi You are a priest forever "like" Melkizedech. Kiingereza inasema "You are a priest forever in the order of Melkizedek". Hili neno "in the order of" ndio limepotea kwenye Kiswahili. Lakini hata kwenye Kiingereza utaona limebadilika kidogo nalo hadi uelewa maana ya "order". Kupata mwanga kidogo hapa inabidi usome Waeb 11:7 ambapo hizi "orders" mbili zinalinganishwa. Kuna "order" ya Aaron na order ya Malkizedeki. Sasa makuhani wa Haruni wao wanapata ukuhani wao kwa kurithi kutoka watoto wa kiume wa Haruni tu. Nisikuchoshe; maana yake kwa ufupi ni kuwa order ya Melkizedeki inashikiliwa na Melkizedeki tu na Yesu mwenyewe. Ndio ukuhani pekee wa kifalme (royal priesthood).
 
Tatizo siyo waraka wa Waebrania, Tatizo ni uelewa wa waraka huo
Nyinyi mnautafsiri out of context kwa kuungaunga maana.

Ngoja Niquote Maandiko

SOURCE: https://www.biblegateway.com/passage/?search=Waebrania+7&version=SNT

Yesu Na Melkizedeki (Waebrania 7:11-17)
11 Kama ukamilifu ungaliweza kupatikana kwa njia ya ukuhani wa Walawi, kwa maana watu walipewa sheria kupitia kwao, ilikuwapo haja gani tena ya kuwepo kuhani mwingine, yaani kuhani kama Mel kizedeki, ambaye si kama Aroni? 12 Kwa maana yanapotokea maba diliko kwenye ukuhani, ni lazima pawepo na mabadiliko katika she ria. 13 Maana Bwana wetu ambaye ndiye anayesemwa katika mambo haya, alikuwa ni wa kabila lingine, na hakuna mtu katika kabila lake aliyewahi kuhudumu katika madhabahu. 14 Inafahamika wazi kuwa Bwana wetu alitoka katika kabila la Yuda, na Mose hakuwahi kusema lo lote juu ya makuhani kutoka katika kabila hilo. 15 Na hili tunalosema linakuwa wazi zaidi anapotokea kuhani mwingine kama Melkizedeki; 16 ambaye ukuhani wake hautokani na kanuni za ukoo wake, bali hutokana na uwezo wa maisha yasiyoharibika. 17 Kwa maana ameshuhudiwa hivi: “Wewe ni kuhani milele, kama wa Melkizedeki.”

Ni dhahiri:
Kwa mujibu wa andiko hilo katika msitari wa mwisho nilioupigia msitari unaosema "WEWE NI KUHANI MILELE KAMA MELKIZEDEKI" inaonysha kuwa YESU ni YESU na MELKIZEDEKI ni MELKIZEDEKI ila wote wana Ukuhani wa Milele!.

Neno "Kama" limetumika kwenye hilo andika KULINGANISHA watu wawili, Nikisema Mtu X kama Mtu Y kwenye ishu Z maana yake siyo kwamba X ndiye Y bali hawa ni watu tofauti lakini wana role Z ambayo ni moja

KITU KIKISHAITWA "KAMA" MAANA YAKE KINAFANANISHWA (compared to) , KINAKUWA SIYO CHENYEWE HALISI!

Ni suala la lugha tu, Ukitaka kutumia logic yako kuungaunga visivyoungika basi bible unaweza kuitafsiri vyovyote unavyopenda na ikaleta justification zozote
Hapa ndipo penye shida watu wakisema Magufuli kama Nyerere wao sijui wanaelewaje!!! kuna tatizo kwenye matumizi ya lugha hii , lakini wafahamu kuwa Magufuli sio Nyerere
Huoni kama wewe ndio una tatizo la uelewa? Unaelewa nini unaposema "out of context?" Mbona hujaanzia aya za mwanzo kwenye nukuu yako? Au umelenga kupotosha kwa kusimamia neno "kama?" Anza mwanzo kabisa mwa hiyo sura ama mlango halafu tuchambue mstari kwa mstari. Karibu
 
hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.

Tunaambiwa huyu ''Jembe'' hakuwa na baba wala mama na anaishi milele hata sasa???

Ukisoma sura yote inamsifia mtu huyu wa ajabu (mysterious) na kusema licha ya ukuu wa Abraham kama Baba wa wayahudi ila haoni ndani kwa huyu Melchizedek!!
Mkuu kwanza thanks for sharing with us hi kitu; miongoni mwa maada ambazo waumini wengi hua wanapata sana TABU basi ni story ya huyu mtu uliyemsema hapa, but kwa kusoma kwangu Biblia, huyu Melkizedeki ni mtu tu kama walivyo pata kua watu wengine, au niweke hivi, Melkizedeki alikua mtumishi wa Mungu kama walivyo pata kutokea wengine na hata waliopo( Yesu anabakia kua ndio kila kitu katika Imani ya Kikristo and may be na zingine ( huko kwingine sina interest nako cause sijasoma sana vitabu vyao) Kwenye huo mstari uliutaja, hebu rudi nyuma mstari 2, utaona imeanza hivi kwa kufungia mabano, "huyo Melkizedeki ( tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena mfalme wa Salem, maana yake mfalme wa Amani; ...inaendelea kama ulivyo copy hapo then akafungia mabano. KWahiyo huyu mtu sio kwamba hakuana na baba wala mama na wala hakua mfalme wa milele bali, tafsiri ya jina lake ndio hiyo. Kwa mfano, jina Emmanuel (jina la kwanza kabisa la ahadi la Yesu ) tafsiri yake ni Mungu pamoja na nasi; Kwa hiyo mtu yeyote aitwaye Immanuel hata leo either ana amini katika Mungu au la, hiyo ndio tafsiri ya jina hilo, hivi unajaua jina Yusufu au Joseph kwa kingereza maana yake ni nini? Ni kwamba mtoa jina ana maana hivi, "God you may give me another son" Haijalishi wazazi wanao toa jina hilo Yusufu/Joseph kwa watoto wao kama na wao wanaomba Mungu afanye hivyo au laa but hio ndio maana yake. So huyu Melkizedeki na yeye jina lake ndio lina tafsiri hiyo but yeye hakua kuahani wa milele na ndio maana hapo hapo ulipotoa maandiko, inasema ni mfano wa….., kitu mfano wa… means sio halisi ila kimebeba kitu kingine.
Again, thanks for sharing na huo ndio mchango wangu
 
Huoni kama wewe ndio una tatizo la uelewa? Unaelewa nini unaposema "out of context?" Mbona hujaanzia aya za mwanzo kwenye nukuu yako? Au umelenga kupotosha kwa kusimamia neno "kama?" Anza mwanzo kabisa mwa hiyo sura ama mlango halafu tuchambue mstari kwa mstari. Karibu
Unataka tuchambue mstari gani !! " KAMA " ni sehemu ya mstari , kama utaki tujadili kilichoandikwa unataka tujadili nini sasa
 
Melkizedeki hakuwa "Kuhani Mkuu" bali "Kuhani wa Mungu aliyejuu sana". Kumbuka wakati huo Mungu aliye juu sana hakuwa amefunuliwa kwa Musa na wala Ukuhani haukuwepo. Lakini tunadokezwa tu kuwa huyu Melkizedeki tayari alikuwa anamtolea sadaka El Elyon (Mwenye Enzi)

Swali zuri sana; itabidi turudi kwenye text yenyewe. Lakini kiufupi ni kuwa Ibrahim alimpa heshima kubwa Melkizedeki na ndio pointi ya baadaye kwenye Waebrania. Kuwa kama Ibrahim alitoa fungu la kumi kwa Melkizedeki ina maana kiwadhifa au hadhi Melkizedeki alikuwa juu yake.

Hili ni swali zuri. Na hapa ndio wengi wanachanganyikiwa. Je, Yesu alikuwepo kabla ya Bikira Maria; au alianza kuwepo baada ya kuzaliwa? Dokezo kidogo ni kuwa katika ile inayojulikana kama "Sala ya Kikuhani" ya Yesu kwenye Yohana 17 tunakutana na ombi hili kwa babake "Na sasa Baba, nitukuze mbele zako kwa ule utukufu niliokuwa nao kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu" (Yoh. 17:5). Na mistari kadhaa chini anasisitiza hili (Yoh. 17:24). Ukisoma mistari hiyo lazima ujiulize? Yesu alikuwepo kabla ya misingi ya ulimwengu? Na kama alikuwepo kuzaliwa kwake na Bikira Maria basi kuna maana gani?
1. Melkizedeki alikuwa kuhani wa Mungu alie juu wala sio kuhani mkuu sawa
2.Ndio Melkizedeki alikuwa juu ya Ibrahim ndio maana akambariki , hili ni jambo la kawaida mkuu ni suala la Mungu tu kumbariki kiumbe wake na kumpa karama nyingi kuliko mwengine

3.Yesu alikuwepo kabla ya msingi wa ulimwengu , hii sikatai lakini njia pekee ya Yesu kujionyesha kwa watu hapa duniani na kuishi nao , ni kuja kuzaliwa na mwanamke , lakini Melkizedeki hii njia ajaipitia kabisa na duniani aliishi na watu bila tabu , vilevile maandiko yanasema huyu Melkizedeki alifananishwa na Mwana wa Mungu lakini Yesu alikuwa mwana wa Mungu kamili , vilevile Melkizedeki alikuwa ni mfalme na kuhani , wakati Yesu alikuwa na vyeo 3(mfalme, kuhani na nabii), ni kweli walifanana lakini sio mtu mmoja
 
Back
Top Bottom