Agano la kale ni kivuli cha Agano jipya. Maana yake yaliyotokea yaliakisi yatakayotokea katika Agano jipya.
Mzee Mwanakijiji kaandika vema nami naandika kwa kiasi.
Tuanze na Yohana 8 ambapo Yesu alikuwa akijibizana na mafarisayo kuhusu Yeye ni nani:
Yohana 8
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁵⁶ Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.
⁵⁷ Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu?
⁵⁸ Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.
Hapa Yesu anatupa dokezo kuwa kuna mahali wakati Ibrahimu akiishi hapa duniani walikutana hivyo basi tukitafuta kwenye Agano la kale tutakuta mahali fulani habari ya Yesu na Ibrahimu. Twende kwenye Agano la kale:
Mwanzo 14
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁸ Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana.
¹⁹ Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi.
²⁰ Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.
Hapa kuna mambo matatu muhimu kumhusu Melkizedeki:
1. Alikuwa mfalme wa Salem
2. Alileta mkate na divai wakala pamoja
3. Alikuwa kuhani wa Mungu aliye juu
Ikumbukwe kuwa katika Biblia yote hakuna mwanadamu aliyetajwa kuwa
mfalme na kuhani kwa wakakati mmoja isipokuwa masihi tu. Tuone andiko moja tu kwa mfano:
Zekaria 6
¹³ Naam, yeye atalijenga hekalu la Bwana; naye atauchukua huo utukufu; ataketi akimiliki katika kiti chake cha enzi; na kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi; na shauri la amani litakuwa kati ya hao wawili.
Ok, tukiangalia hayo mambo matatu, salem (shalem kwa kiebrania) sio mahali, bali ni ufafanuzi. Maana yake ni amani, hivyo alikuwa mfalme wa AMANI, sifa ambayo imetajwa kuwa nayo masihi pekee.
Isaya 9
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁶ Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.
Alileta mkate na divai ambayo ni komunyo. Angalia jambo hilo lilifanyika pia kwenye Agano jipya.
Tuangalie sasa Waebrania:
Waebrania 7
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;
² ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;
Kumbe hata neno Melkizedeki sio jina kama tulivyodhania, ni maelezo tu. Melkizedeki = mfalme wa haki. Yesu ndiye atakayehukumu kwa haki, yeye ni mfalme wa haki pia mfalme wa amani.
³ hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.
Nadhani umeona
parallel iliyopo kati ya Agano la kale na jipya, hicho ndicho kivuli kilichokuja kudhihirika kwa Agano jipya.
Kama hujaelewa uliza.