Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Huielewi bible na hutoweza kumwelewa Paulo maana na yeye alikuwa great thinker.Watu waliomezeshwa huwa wanabisha hadi facts.
Ngoja nikuonyeshe uone James, ndugu yake Yesu na Mwanafunzi wa Yesu alimuonaje Paulo
Paulo anasema kwenye kitabua cha Warumi kama ifuatavyo kwenye Warumi (4: 1-3)
4 usemeje basi kuhusu baba yetu Abrahamu? Yeye alijifunza nini?2 Ikiwa Abrahamu alihesabiwa haki kwa matendo, basi anacho kitu cha kujivunia, lakini si mbele za Mungu. 3 Maandiko yanase maje? “Abrahamu alimwamini Mungu na kwa ajili ya imani yake aka hesabiwa haki.”
Source :
https://www.biblegateway.com/passage/?search=warumi+4&version=SNT
Hapo Paulo anasisitiza Imani kuwa Yatosha na kwamba Matendo si hoja sana mbele ya Mungu
Chini hapa nakuwekea Majibu ya James ndugu yake Yesu, kwenye kitabu cha James (Kwa Mujibu wa King James Version(KJV) na New International version (NIV), kinaitwa James) ila kwa ajili yako wewe Mswahili wamekubadirishia hadi jina la kitabu badala ya Kukiita kitabu cha James wamekiita kitabu cha Yakobo, sijui walitaka kutuficha nini sisi waswahili [Hili ni somo jingine ngoja nisiingize mada ndani ya mada] 😀 😀
Yakobo 2:20-23 Inasema:
Ewe mpumbavu, unataka ushahidi wa kuthibitisha kwamba imani bila matendo ni bure? 21 Je, Abrahamu baba yetu hakuhesa biwa haki kwa matendo, alipomtoa mwanae Isaki madhabahuni? 22 Unaona jinsi ambavyo imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake na imani ikakamilishwa kwa matendo. 23 Kwa njia hiyo yaka timizwa yale Maandiko yasemayo, “Abrahamu alimwamini Mungu, na kwa imani yake akahesabiwa kuwa mtu mwenye haki”; naye akaitwa rafiki wa Mungu.
Source:
Bible Gateway passage: Yakobo 2 - Neno: Bibilia Takatifu
Onyo Kuhusu Upendeleo -Ndugu zangu wapendwa, msiwe na upendeleo mnapoishika imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu. Tuseme mtu mmoja aliyevaa pete ya dhahabu na nguo maridadi anakuja katika mkutano wenu; kisha fukara mmoja mwenye nguo chafu na mbovu akaingia pia. Ikiwa utamshughulikia...
Kwa Kiingereza(Kutoka New International Version) kitabu hicho hicho ambacho sasa kinakwenda kwa jina la James kinasema:
James 2: 20-23
20 You foolish person, do you want evidence that faith without deeds is useless[d]? 21 Was not our father Abraham considered righteous for what he did when he offered his son Isaac on the altar? 22 You see that his faith and his actions were working together, and his faith was made complete by what he did. 23 And the scripture was fulfilled that says, “Abraham believed God, and it was credited to him as righteousness,”[e]and he was called God’s friend. 24 You see that a person is considered righteous by what they do and not by faith alone.
Source: https://www.biblegateway.com/passage/?search=James+2&version=NIV
UMEONA MANENO MAKALI AMBAYO JAMES NDUGU YAKE YESU ANAMTOLEA PAULO KWA MAFUNDISHO YAKE?
Hapo sijagusia jinsi James alivyomtega Paulo kuhakikisha anafuata sheria za Kiyahudi mbele ya kadamnasi ya Wayahudi ili kuthibitisha kama kweli anasimamia misimamo yake ya kuwa "tumefunguliwa kutoka katika minyorro ya torati ya Musa, au Sharti mwanafunzi wa Yesu aendee kutii Torati?
Kwa Taarifa zako Paulo siku hiyo hakuwa na jinsi ilibidi afuate ritual zote za Wayahudi la sivyo hakuna Myahudi ambaye angemchukulia serious kabisa na mafundisho yake!
Soma Biblia ndugu uelewe, usikubali kupelekwa pelekwa