Hongera ila nilijua mnazindua tayari imetengenezwa, kumbe ndio mnajiandaa kutengeneza, hivi ni kipi mumetengeneza au mradi gani mumekamilisha maana naona kila sehemu na kila siku ni uanzishwaji wa miradi, lini mtakamilisha hata moja muitumie kwenye picha za kampeni, mumesalia na mwaka mmoja muingie kwenye uchaguzi.
Kuna ile SGR mnatupigiaga makelele humu kila siku nilijua mshapiga hatua mpo mnakamilisha, juzi ndio nimeona humu mumeanza kutupa mapicha ya ulazaji wa mataluma ya zege, yaani bado mbali sana, ilhali ni kasafu kenye umbali mdogo sana kilomita 200km wakati sisi tumechana mbuga tupo mbali sana.